Mafuriko: Adha ya mvua pwani ya Kenya

Maelezo ya sauti, Mafuriko yadaiwa kuhatarisha maisha ya wakazi nchini Kenya

Maeneo kadha wa kadha nchini Kenya hutazama mvua kama baraka kwa kuwa maji yatokanayo na mvua hizo ni muhimu kwa matumizi ya binaadamu, hasa kwa ajili ya umwagiliaji kwenye mazao.Lakini tayari wengine wamelalamika kuhusu mafuriko yatokanayo na mvua hizo zinazodaiwa kuhatarisha maisha ya wakazi.

Jamhuri Mwavyombo amezungumza na Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Mazingira Kaunti ya Mombasa Steven Wambua kuhusu hali hiyo