Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.10.2018: Mourinho, Zidane, Foden, Zabaleta, Ashley
Kocha wa Manchester United,Jose Mourinho anaweza kufukuzwa mapema wiki ijayo kama timu yake itafungwa na Newcastle United siku ya Jumamosi. (Sun)
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino ndio anategemewa kuchukua nafasi ya kuwa kocha wa Manchester United kama Mourinho atafukuzwa. (Independent)
Mlinda mlango wa Manchester United David De Gea, kiungo wa kati Paul Pogba na mshambuliaji Anthony Martial walikuwa wanatahitajika na Zinedine Zidane wakati akiwa meneja wa Real Madrid. (Manchester Evening News)
Mlinzi wa kati wa Chelsea Antonio Rudiger, 25, anaamini kwamba Eden Hazard ndio mchezaji mahiri zaidi katika timu ya Blues inayoongozwa na Maurizio Sarri. (Standard)
Mshambuliaji wa Manchester City Benjamin Mendy, 24,anasema mazoezi makali anayopewa na meneja Pep Guardiola yanamfanya kuwa bora zaidi. (Manchester Evening News)
City watatumia kamera ya kiwango cha juu ili kuwapeleleza wachezaji wake wakiwa katika basi katika mechi ya Jumapili watakayocheza na Liverpool baada ya gari walilopanda msimu uliopita kushambuliwa kwa mawe.(ESPN)
Wakati huo huo kiungo wa kati kinda wa City Phil Foden, 18 amenunua nyumba ya £ milioni 2 kwa ajili yake na familia yake kwa lengo la kuimarisha umoja wao licha ya umaarufu aliokuwa nao. (Mail)
Timu ya Arsenal inajaribu kumuwania meneja mkuu wa Jeventus, Giuseppe Marotta ambaye anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo lakini Inter Mian pia imeonyesha nia.
Meneja wa zamani wa England Fabio Capello amesema ameambiwa na meneja wa Manchester United Jose Mourinho kuwa alitaka kumsajili Milan Skriniar ,23, kutoka Inter Milan na Kalidou Koulibaly ,27,wa Napoli msimu uliopita. (Sky Italia via Football.London)
Mmiliki wa Newcastle,Mike Ashley amehaidi kuwapeleka wachezaji wake likizo kama hawatoshuka daraja EPL. (Mail)
Ashley anadaiwa kula tambi za £ 7.95 wakati akiwa katika kikao cha muda wa saa nne akiwa na meneja Rafa Benitez na wachezaji wiki hii. (Chronicle)
Mlinzi wa Sweden na Helsingborgs IF Andreas Granqvist, 33, anasema alikuwa anatania katika uvumi unaosambaa unaomuhusisha yeye na Manchester United. (FotbollDireckt via Manchester Evening News)
Meneja wa zamani Manchester United na Everton David Moyes yuko kwenye nafasi nzuri ya kuchukua pahala pa Steve Bruce ya kuwa meneja wa Aston Villa. (Express)
Mshambuliaji wa Fiorentina Giovanni Simeone, 23,amebainisha matumaini yake kuwa siku moja anaweza kuwa meneja kama baba yake Diego ambaye ni kocha mkuu wa Atletico Madrid. (Goal)
Bora kutoka Alhamisi
Mshambuliaji wa Monaco na Colombia Radamel Falcao, 32, amehusishwa na kuhama kwenda klabu ya David Beckham ya Inter Miami wakati timu hiyo itajiunga na MLS mwaka 2020. (Sport)
Gareth Southgate atasaini mkataba ndani ya saa 24 zinazokuja kusalia kama meneja wa England hadi mwaka 2022. (Mirror)
Mkataba huo ambao unaripotiwa kuwa wa thamani ya paunia milioni 3 kwa mwaka, utamweka kwenye klabu meneja huyo mwenye miaka 48 hadi baada ya Kombe la Dunia nchini Qatar.
Manchester City wamefanya mikutano kadhaa na polisi huko Merseyside na huenda wakaweka siri njia ambayo watatumika siku ya Jumamosi na Liverpool huko Anfield kuzuia kurudia kile kilichotokea mismu uliopita wakati wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa. (Sun)
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, amekataa ofa ya tatu ya thamani ya pauni milioni 6.38 kuongeza mkataba wake kwenye klabu hiyo. (Bein Sport)
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na naibu meneja wa Ubelgiji Thierry Henry pia naye anataka kazi huko Aston Villa. (Mirror)
Lakini aliyekuwa nyota wa Chelsea John Terry ambaye alicheza huko Villa Park mwaka uliopita pia anatajwa kuwa huenda akapata kazi yake ya kwanza ya umeneja. (Sun)