Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 04.10.2018: Southgate, Falcao, Rabiot, Fonseca, Isco, Henry

Mshambuliaji wa Monaco na Colombia Radamel Falcao, 32, amehusishwa na kuhama kwenda klabu ya David Beckham ya Inter Miami wakati timu hiyo itajiunga na MLS mwaka 2020. (Sport)

Gareth Southgate atasaini mkataba ndani ya saa 24 zinazokuja kusalia kama meneja wa England hadi mwaka 2022. (Mirror)

Mkataba huo ambao unaripotiwa kuwa wa thamani ya paunia milioni 3 kwa mwaka, utamweka kwenye klabu meneja huyo mwenye miaka 48 hadi baada ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Wamiliki wa Manchester United, familia ya Glazer bado wanamuunga mkono Jose Mourinho kama meneja wa klabu licha ya nafasi hiyo kutiliwa shaka kufuatia matokeo mabaya ya United ya kuanza kwa msimu. (ESPN)

Manchester City wamefanya mikutano kadhaa na polisi huko Merseyside na huenda wakaweka siri njia ambayo watatumika siku ya Jumamosi na Liverpool huko Anfield kuzuia kurudia kile kilichotokea mismu uliopita wakati wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa. (Sun)

Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23, amekataa ofa ya tatu ya thamani ya pauni milioni 6.38 kuongeza mkataba wake kwenye klabu hiyo. (Bein Sport)

Meneja wa Shakhtar Donetsk, Paulo Fonseca ni mmoja wa wale wanaweza kuchukua nafasi huko Aston Villa baada ya Steve Bruce kufutwa siku ya Jumatano. (Birmingham Mail)

Mchezaji wa zamani wa Arsenal na naibu meneja wa Ubelgiji Thierry Henry pia naye anataka kazi huko Aston Villa. (Mirror)

Lakini aliyekuwa nyota wa Chelsea John Terry ambaye alicheza huko Villa Park mwaka uliopita pia anatajwa kuwa huenda akapata kazi yake ya kwanza ya umeneja. (Sun)

Aliyekuwa meneja wa Hull City Paul Duffen anaongoza kundi ambalo linataka kununua klabu kutoka kwa mmiliki wa sasa Assem Allam. (Hull Daily Mail)

Mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour angeinunua Newcastle United badala ya Man City miaka 10 iliyopita. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 26, anasema anakaribia kupona kabisa baada ya kufanyiwa upasuaji. (AS)

Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll anatarajiwa kutejae baada ya kupata jeraha. Hajaichezea Hammers tangu mwezi Mei. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Chelsea Ross Barkley anasema alikosa kufanya kazi kama kocha akiwa na Everton na kuwa sasa ni wakati mwafaka kuondoka kwenye klabu hiyo. (Liverpool Echo)

Bournemouth wanafikiria kumwendea kiungo wa kati wa SPLA na Italia mwenye miaka 24 Manuel Lazzari. (Calciomercato)

Bora zaidi kutoka Jumatano

Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 25. (The Sun)

Kiungo wa kati zamani wa Manchester United Paul Scholes, 43, anasema ameshangazwa kuwa meneja Jose Mourinho hakufutwa baada ya kushindwa kwa mabo 3-1 na West Ham siku ya Jumamosi. (BT Sport)

Mshambuliaji Mfaransa Christophe Dugarry anasema kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 46, mchezaji mwenzake wa zamani wa kimataifa hawezi kuchukua mahala pake Mourinho huko Old Trafford. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Mshambuliajia wa Arsenal Danny Welbeck anatarajiwa kumfuata kiungo wa kati Aaron Ramsey kuondoka Arsenal msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27 wa kimataifa wa England yuko katika mwaka wake wa mwisho na hakuna makubaliano kuhusu mkataba wake mpya. (Mirror)

Mshambuliajia wa Arsenal Danny Welbeck anatarajiwa kumfuata kiungo wa kati Aaron Ramsey kuondoka Arsenal msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27 wa kimataifa wa England yuko katika mwaka wake wa mwisho na hakuna makubaliano kuhusu mkataba wake mpya. (Mirror)