Tetemeko Indonesia: Maeneo yaliyoathirika yafikiwa na huduma ya kwanza, idadi ya waliofariki yaongezeka

Chanzo cha picha, AFP
Maafisa nchini Indonesia wamesema kuwa wameweza kufikia wilaya zote nne zilizoathiriwa na tetemeko na tsunami mwishoni mwa juma lililopita katika kisiwa cha Sulawesi.
Lakini katika baadhi ya sehemu ni idadi ndogo ya vikosi vya uokoaji vimefika.
Misaada inapelekwa katika sehemu zilizoathiriwa, lakini wanakumbana na changamoto kubwa kutokana na kuharibika kwa miundombinu.
Mpaka sasa zaidi ya watu 1,347 wamethibitishwa kufariki huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa zaidi ya watu laki mbili walionusurika katika tukio hilo wanahitaji msaada wa haraka.

Hali hii inajulikana kama Strike-slip, ambayo inaweza kusababisha mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 ambayo yaligonga fukwe za mji wa Palu na kumshangaza kila mmoja.

Chanzo cha picha, AFP
Kumbuka kuwa ili kuwepo mawimbi kama hayo ni lazima kuwe na kusonga kwa kiwango kikubwa cha sakafu ya bahari, kitu ambacho kinasababisha maji kusonga kwenda kila upande.
Hesabu za awali zinaonyesha kusonga kwa sakafu ya bahari kwa hadi nusu mita lakini hilo halingeweza kusababisha mawimbi yaliyorekodiwa.
Licha ya kufikia sehemu hizi zilizoathiriwa vibaya, changamoto kubwa inabaki ni namna gani majumba makubwa yaliyoporomoka yanaweza kuondolewa na kupata watu walionasa ndani yake?

Chanzo cha picha, AFP
Jan Egeland kutoka shirika la wakimbizi nchini Norway na ambaye alikua katika kamati ya maafa ya tsunami ya mwaka 2004 nchini humo ambayo iliua zaidi ya watu laki mbili kutoka eneo la bahari ya Hindi. Anasema kupeleka misaada ya kimataifa sehemu kama hizo ni jambo gumu sana.

Chanzo cha picha, PLANET
Huku haya yote yakiendelea, idadi ya watu waliofariki inatarajiwa kuongezeka na kufikia zaidi ya idadi ya sasa ambayo ni 1350.
Je unajua tsunami zinavyotokea?













