Tetemeko la ardhi Indonesia: Watu 380 wauwawa na wengine maelfu kujeruhiwa

Indonesia's disaster agency said some people scaled trees to escape the huge waves

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu wengine walijiokoa kwa kupanda kwenye miti

Watu zaidi ya 380 wamethibitishwa kufa baada ya tsunami kusababisha tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 7.5 lilopiga mji wa Indonesia hapo jana.

Upepo mkali ulivuma kutoka Palu katika kisiwa cha Sulewesi kwa mita 3.

Video inayoonekana kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha jinsi watu walivyokuwa wakipiga kelele huku wakikimbia kwa hofu.

Baada ya mshtuko wa tetemeko hilo, maelfu walizimia majumbani kwao na wengine wakielekea hospitalini ,hotelini na kwenye maduka makubwa.

Jitihada za uokoaji zinaendelea ingawa zimepata changamoto ya umeme kuwa umekatika.Njia kuu ya Palu imefungwa kutokana na daraja kuu kuanguka pia.

Nyumba,hoteli

Chanzo cha picha, Reuters

Miili mingi imepatikana katika ufukwe

Mamlaka ya maafa nchini Indonesia imesema, watu wapatao 384 wamekufa ingawa idadi inategemewa kuongezeka na watu 540 wamejeruhiwa.

Watu zaidi ya 380 wamethibitishwa kufa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watu zaidi ya 380 wamethibitishwa kufa

Miili mingi ilikutwa ufukweni kwa sababu ya tsunami lakini idadi yake bado haijafahamika.

Msemaji wa serikali ,Sutopo Purwo Nugroho aliiambia Reuters kuwa wakati onyo lilipotolewa hapo jana watu waliendelea na shughuli zao ufukweni na hawakuchukua tahadhari ya kukimbia mara moja hivyo wakawa miongoni mwa wahanga.

Wengine waliokoka kwa kupandia katika miti ili kukimbia upepo mkali.

Tetemeko hili lilianza kwa kutangulia kwa tetemeko lingine dogo liliuwa mtu mmoja na wengine 10 kujeruhiwa wakiwa katika soko dogo la samaki huko Donggala.

Mjini Palu,Mamia ya watu walikuwa wanajiandaa kwa ajili ya tamasha lililokuwa linatarajiwa kuanza ijumaa jioni.

This hospital in Palu collapsed in the earthquake

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Hospitali kuu ya Palu iliathirika na tetemeko la ardhi pia

Hospitali kuu imeharibiwa na tetemeko la ardhi hivyo watu wengi imewabidi kupata huduma wakiwa nje .

Huduma za afya zinatolewa nje

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Huduma za afya zinatolewa nje

Palu na Donggala ni miji yenye makazi ya watu zaidi ya 600,000.Rais wa nchi hiyo Joko Widodo amesema makundi ya waokoaji yanaendelea kuelekea katika sehemu iliyopata janga ili kutoa msaada zaidi.

Uwanja wa ndege wa Palu umefungwa kutokana na tsunami ingawa helikopta zitaendelea kufanya kazi.

Ndege za jeshi ndio zinatumika kuendelea kutoa msaada

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ndege za jeshi ndio zinatumika kuendelea kutoa msaada

Jeshi la nchi hiyo litatuma ndege za jeshi kutoka mji mkuu wa Jakarta.

Mamlaka ya hali ya hewa ya Indonesia inalaumiwa kwa kuchelewa kutoa angalizo kwa sababu onyo juu ya tsunami lilitolewa ndani ya saa moja kabla ya tsunami kupiga.

raman

Inakumbukwa kuwa mwaka 2004 tsunami ilisababisha tetemeko la ardhi nchini Indonesia na watu zaidi ya laki mbili walifariki.

Mwaka 2010 pia zaidi ya watu 282 waliuawa na tsunami iliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika pwani ya Sumatra nchini Indonesia.