Tetemeko la ardhi Indonesia: Indonesia yaomba msaada wa kimataifa, Thailand na Australia zapeleka vifaa vya usaidizi

A shattered mosque in Palu, 30 September

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Msikiti huu Palu uliharibiwa na tsunami

Indonesia imeomba msaada wa jumuiya za kimatafa wakati huu ikihangaika kupata chakula sambamba na vifaa vya uokoaji katika kisiwa cha Sulawesi, ambacho kimeharibiwa vibaya kwa kimbunga na tsunami mwishoni mwa juma lililopita.

Thailand na Australia ni miongoni mwa nchi ambazo tiyari zimetoa misaada yao.

Vikosi vya uokoaji vinaendelea na juhudi za kutafuta watu waliokwama katika majumba makubwa kwenye mji wa Palu huku uwezekano wa kuwakuta wakiwa hai ukiendelea kupungua.

Tetemeko hilo lilichangia kutokea kwa tsunami yenye mawimbi ya hadi urefu wa miata 6.

Waokoaji wamekuwa wakichimba kwa mikono wakiwatafuta manusura kwenye mji wa Palu.

Vikosi vya uokoaji vinajaribu kuwafikia mamia ya watu ambao inawezekana wakawa hai katika mji wa Palu ambao miundombinu yake imeharibika vibaya huku wengi wao wakitajwa kukwama katika maduka na majumba makubwa.

Sehemu kubwa ya mji wa Palu imeharibiwa vibaya huku dalili za kuwapata walionasa wakiwa hai zikianza kufifia.

Watu wakifukia kaburi

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, Watu wakifukia kaburi

Katika ziara yake kwenye mji wa Palu Rais wa Indonesia Joko Widodo, amewaambia viongozi wa eneo hilo kuwa serikali kuu itatoa mahitaji yote muhimu ili matengenezo mapya ya mji huo yaweze kufanyika.

''Hakika hii ni hali ya dharura kama ilivyo ya Lombok. Kutakua na ugumu wakati, kwa siku moja au mbili na ni kazi kubwa. Uelekeo wa Barabara hii haipo imefungwa, ata uwanja wa Ndege haufanyi kazi ipasavyo," amesema.

"Vituo vya kuzalisha umeme pia vimeharibiwa, na kati ya saba ni viwili tu ndivyo bado vinafanya kazi na wasambazaji wa mafuta wasingeweza kuyafikia maeneo kutokana na kuharibika kwa barabara. Lakini tayari tumeagiza kila kitu kama mafuta, na wasambazaji watafika siku mbili kuanzia sasa.

"Na vifaa vyote vizito vitakuja usiku wa leo, ili tuweze kuvitumia kesho pamoja na ahueni ya misaada kama vile chakula na maji safi.Baada ya kuona kila kitu kinafanya kazi kama kawaida tutaingia kwenye hatua kujenga na kuzirekebisha nyumba hizo. Na Serikali itawaaidia kama tukivyofanya Lombok."

Palu map
Maelezo ya picha, Ramani ya Palu

Kuna wasi wasi kuhusu hali ya mji wa Donggala ambopo kiwango cha uharibifu bado hakijulikani.

Shirika la msalaba mwekundu limekuwa likikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wameathiriwa na tetemeko hilo la ardhi na tsunami lililotajwa kuwa janga ambalo litazidi kuwa baya zaidi.

Makamu rais nchini Indonesia Jusuf Kalla alisema idadi kamili ya watu waliouawa inaweza kufika maelfu.

A tsunami-devastated area in Talise beach, Palu, central Sulawesi, Indonesia, 30 September 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Tsunami iliacha uharibifu mkubwa

Mitetemeko midogo ya ardhi imekuwa ikiendelea kupiga kisiwa hicho tangu siku ya Ijumaa.

Baadhi ya manusura wamesema walisukumwa zaidi ya mita 500 na mawimbi yaliyoambatana na kimbunga hicho. Baadhi walikuwa na watoto wao pamoja na wapendwa wao lakini mwishoni wakajikuta wapo wenyewe.

Serikali imelimarisha jeshi na raia wauokoaji ili kusaidia kuondoa miili ya watu walioangukiwa na majengo na wale ambao bado wapo ndani ya majengo hayo wakisikika kuomba msaada.

Rais Joko Widodo yuko Palu na anakagua maeneo yaliyoathiriwa na janga hili zikiwemo fukwe za Talise, eneo kuu la kitalii lililoathiriwa vibaya na tsunami.

Miili imekuwa ikitabakaa kwenye mitaa ya mji na waliojuhiwa wanatibiwa kwenye mahema kwa sababu hospitali ziliharibiwa.

Walionusurika mjini Palu walilala nje siku ya Jumamosi kufuatia onyo la kuwatahadharisha wasirudi makwao.

Rubble of the Roa Roa hotel in Palu

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Watu wengi walikuwa kwenye hoteli hii ya Roa Roa na baadhi walifukiwa kwenye vifusi