Sulawesi: Ni kwa nini tsunami ya Indonesia imewakanganya wanasayansi?

Quake damage

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Tetemeko lilikuwa kubwa lakini sio lile linahusishwa na tukio kubwa la tsunami

Janga la siku ya Ijumaa la tsunami katika kisiwa cha Sulawesi ni kitendawili kwa wengi.

Wakati huduma za dharura zikishika kasi, wanasayansi wanajikuna vichwa kujaribu kuelewa ni kwa nini mawimbi makubwa kama hayo yakatokea.

Tetemeko hilo la ukubwa wa 7.5 katika vipimo vya Richter - ni moja ya yale makubwa kuwai kurekodiwa popote pale duniani mwaka huu.

Lakini hiki ni kile wanasayansi wanasema kuwa hutokea wakati ardhi hupasuka. Katika hali kama hii jiwe la mashariki husonga kwenda kaskazini.

Palu map
Maelezo ya picha, Ramani ya Palu

Hali hii inajulikana kama Strike-slip. ambayo inaweza kusababisha mawimbi ya hadi urefu wa mita 6 ambayo yaligonga fukwe za mji wa Palu na kumshangaza kila mmoja.

Kumbuka kuwa ili kuwepo mawimbi kama hayo ni lazima kuwe na kusonga kwa kiwango kikubwa cha sakafu ya bahari, kitu ambacho kinasababisha maji kusonga kwenda kila upande.

Hesabu za awali zinaonyesha kusonga kwa sakafu ya bahari kwa hadi nusu mita lakini hilo halingeweza kusababisha mawimbi yaliyorekodiwa.

Kwa hivyo ni kipi kilitokea? Mambo mawili yanaibuka kuwa chanzo.

Kwanza kuna shaka kuwa huenda tetemeko hilo la ardhi lilisababisha aina fulani ya maporomoko ya ardhi chini ya bahari.

Tsunami damage

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Uharibifu za tsunami

Katika sehemu zenye milima, mawe na kuporomoka kwa ardhi ni kati ya vitu ambavyo hutokea sawa na majengo yaliyoporomoka. Lakini chini ya bahari kusonga kwa bahari kunaweza kuwa chanzo cha kutokea majanga ya tsunami.

Wakati haya yakifanyika kawaida mawimbi ambayo hugonga fukwe ni makubwa.

Hiki huenda ndicho kilitokea siku ya Ijumaa na mawimbi hayo yakachochewa na umbao la eneo hilo la Palu lenyewe.

Jamii ya wanasayansi vile tunavyoongea inajaribu kubaini na kuelewa kile kilichotokea.

Palu city before and after

Chanzo cha picha, PLANET

Maelezo ya picha, Picha za satelaiti zinaonyesha taka ikisombwa upande fulani

"Hesabu zangu za kwanza za mabadiliko ya sakafu ya bahari ni sentimita 49," alisema Dr Mohammad Heidarzadeh, naibu profesa wa uhandisi wa maeneo ya pwani katika chuo cha Brunel nchini Uingereza.

"Kutokans na hilo unaweza kutarajia tsunami ya chini ya mita moja, na sio mita sita. Kwa hivyo kuna kitu kingine kinafanyika,

Kila kitu ni lazima kibainike siku zinazokuja wakati watafiti wanaingia eneo hilo kuona athari za tetemeko la ardhi na tsunami.

Setilaiti za dunia pia nazo zina jukumu la kutoa picha nyingi iwezekanavyo. Lakini hili litakuwa gumu kwa sababu sulawesi iko katika equator na kuna uwezekano wa kuwepo mawingu mengi angani yanayoweza kuzuia kamera.

Larger view

Chanzo cha picha, PLANET

Maelezo ya picha, Picha inaonyesha kusombwa kwa mitaa