Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dar es Salaam ni mji wa pili kwa utajiri Afrika mashariki baada ya Nairobi, Tanzania na Kenya zinatajirika kwa kasi
Dar es Salaam ni mji wa pili Afrika mashariki kwa utajiri baada ya Nairobi, ambapo kwa jumla Afrika ni mji wa 12 na Nairobi mji wa sita.
Mombasa ni mji wa 23 kwa utajiri Afrika.
Tanzania kama taifa ni ya nane kwa jumla ya utajiri wa raia wake barani Afrika, ambapo Kenya inashikilia nafasi ya tano.
Kwa mujibu wa ripoti ya New World Wealth pamoja na benki ya AfrAsia nchini Mauritius, utajiri wa Dar es Salaam wenye thamani ya $25 bn mwaka 2017 umetokana miongoni mwa mengine na viwango vya utajiri wa watu binafsi (HNWIs) na pia katika mapato yanayoingia katika sekta ya starehe barani Afrika kama hoteli na vivutio vingine.
Hii ni hatua iliyopigwa ikilinganishwa na utajiri wa thamani ya $23bn kwa nchi nzima ya Tanzania mnamo mwaka 2011.
Kwa jumla ripoti hiyo inakadiria kuwa sekta hiyo ya starehe barani Afrika imechangia takriban $ bilioni 6.0 za mapato mnamo 2017.
Kwa kuangazia kiwango cha ongezeko la utajiri, mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, isipokuwa Burundi, ni miongoni mwa nchi ambazo zimeimarika pakubwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Mauritius inaongoza kwa ukuaji wa asilimia 192 ikifuatwa na Ethiopia iliyokuwa kwa asilimia 190.
Baada ya hapo, mataifa ya Afrika Mashariki yanafuata yakiongozwa na Rwanda (74%), Kenya (73%), Tanzania (66%), na Uganda (53%).
Na takwimu hii inajumuisha vitu kama : Magari na nguo za kifahari, ndege za kibinfasi, maboti , na hoteli zinazomilikiwa.
Afrika kusini ndiyo kivutio kikuu cha utalii Afrika, lakini Tanzania inasifika pakubwa kwa vivutio vikiwemo: Ngorongoro, mbuga ya Serengeti.
Na hii ni kama ilivyo kwa mfano wa Masai Mara nchini Kenya, na safari za kuzuru milima ya Virunga na msitu wa Bwindi nchini Uganda kwenda kutazama sokwe.
Dar es Salaam ni mojawapo ya miji inayotazamwa kukua kwa kasi duniani.
Kuihusu Tanzania
Kwa mujibu wa Jacque Morisset, mwanauchumi mkuu wa benki ya Dunia, wakaazi wa Dar es Salaam kwa jumla wanaonekana kumiliki mali zaidi ya watu wanaoishi nje ya mji huo na hasaa katika maeneo ya mashambani.
Mji wa Dar es Salaam una mali ya kibinfasi inayomilikiwa yenye thamani ya mamilioni ya dola ukifuatwa na Kampala, na Mombasa, uliopo pwani ya Kenya ambayo ina na mali ya mamilioni ya dola, yalioekezwa zaidi katika hoteli na nyumba za mapuzmiko za kifahari katika fukwe za bahari.
Utajiri dhidi ya Umaskini
Licha ya haya bado changamoto inasalia katika mgawanyiko wa uchumi wa taifa unaoegemea upande mmoja zaidi.
Kiwango kidogo cha matajiri ikilinganishwa na sehemu kubwa ya watu walio maskini katika mji mkuu huo.
Picha iliopo ni ya badhi walio maskini wanaoishi katika mitaa inayokosa huduma muhimu kama maji.
Huku upande wa pili wachache walio na mali wakiwa na uwezo wa kuishi katika nyumba za ufukweni zenye thamani ya mamilioni ya dola au wengine katika mitaa ya kifahari katika wilaya zilizopo kaskazini.
Ripoti hiyo imetathmini utajiri, starehe, mkondo wa umiliki na usimamizi wa mali barani Afrika kati ya mwaka 2007 hadi 2017, ikitazamia makadirio ya hadi 2027.
Na imefanya hesabu ya utajiri wa kila nchi kutokana na idadi ya wananchi wanaofanya kazi au kuishi ndani ya nchi hiyo.
Katika mji mkuu wa nchi jirani Kenya, Nairobi huvutia watu wenye utajiri katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Mji uliopo pwani Mombasa una umaarufu wa kuvutia watalii katika hoteli nyingi zinazopatikana ufukweni mwa bahari hindi na maeneo yalio torathi za kitaifa na vivutio vikuu duniani .
Nchini Uganda na Rwanda, utajiri wa watu binafsi umetajwa kuogezeka kwa 6% huku Tanzania ikiwa ni 5% kwa jumla nchini.