Rais George Weah amtuza aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsène Wenger

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Liberia George Weah amemtuza aliyekuwa meneja wa klabu ya Arsenal, Arsène Wenger na tuzo ya hadhi ya juu zaidi nchini Liberia kwenye sherehe iliyoandaliwa kwenye mji mkuu Monrovia.
Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.

Chanzo cha picha, EPA
Weah ndiye mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la Fifa la mchezaji wa mwaka. Alistaafu kutoka soka mwaka 2003 na kuingia siasa.
Lakini ya hatua ya Wenger kutuzwa hatua hiyo imezua maoni tofauti nchini humo.
Baadhi wanasema kuwa tuzo hiyo haistahili kupewa mtu binafsi kwa kile amemfanyia rais pekee.

Chanzo cha picha, EPA
Lakini tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wenger amechangia kwa michezo barani Afrika na kuwapa waafrika wengi fursa kwa mujibu wa waziri wa habari.
Rais Weah amesema kuwa Wenger "alinitunza kama mtoto wake" wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa "kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya".

Chanzo cha picha, Getty Images








