Ukungu watatiza safari za ndege kwa muda Kenya

Muda wa kusoma: Dakika 1

Ndege kadhaa zilitatizika kutua katika uwanja mkuu wa ndege Nairobi hii leo kutokana na ukungu mkubwa uliotanda asubuhi.

Baadhi zililazimika kugeuza njia kuelekea katika viwanja vingine vya ndege kutokana na hali hiyo ya hewa iliofanya kuwa vigumu mtu kuona mbele kutokana na ukubgu huko.

Baadhi ya wasafiri walichelewa kufika na baadhi safari zao kutatizika kwa waliokuwa wakiunganisha safari au kubadili ndege kuingia nyingine kutoka uwanja huo wa JKIA.

Ndege kadhaa zilizotarajiwa kutua Nairobi zilibidi kuelekezwa kwingine ikiwemo Mombasa, Pwani ya Kenya.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter shirika la ndege la Kenya Airways, limesema usafiri wa ndege umetatizika kutokana na hali bali ya hewa iliotatiza marubani kuona vizuri.

Lakini sio tu kwa viwanja vya ndege baadhi ya watu walilamika katika mitandao ya kijamii namna hali hiyo ya hewa ilivyowaathiri usafiri wa barabarani:

Kenya Airways inamilikiwa kwa 48.9% naserikali na 7.8 % na kampuni ya ndege Air France-KLM.

Ndege 25 za nchi za nje huhudumu nje ya uwanja mkuu wa ndege Nairobi, ikiwemo Turkish Airlines, Emirates, South African Airways na Ethiopian.