Vitabu ambavyo Obama angependa usome kwa sasa vilivyoandikwa na Waafrika

Uhuru Kenyatta na Bw Obama Ikulu, Nairobi

Chanzo cha picha, UHURU KENYATTA/TWITTER

Maelezo ya picha, Uhuru Kenyatta na Bw Obama Ikulu, Nairobi

Wiki hii ninasafiri kwenda Afrika kwa mara ya kwanza tangu nitoke ofisini, bara la mambo mazuri, tamaduni nzuri na hadithi za kupendeza, Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Kwa miaka iliyopita nimevutiwa na fasihi isiyo ya kawaida kutoka nchi za Afrika. Ninapojiandaa kwa safari hii ningependa kutangaza vitabu ambavyo unaweza kuvisoma msimu huu wa joto vikiwemo kutoka kwa waandishi bora zaidi wa Afrika, aliandika Obama.

Vitabu hivyo ni vifuatavyo:

Things Fall Apart cha Chinua Achebe

Things Fall Apart na Chinua Achebe

Chanzo cha picha, Hisani

Maelezo ya picha, Things Fall Apart na Chinua Achebe

Kitabu hiki kinatoa picha ya jamii ya kitamaduni inayopambana na kuwasili kwa mambo ya kigeni kutoka kwa wamishenari wa kikiristo hadi kwa wakoloni kutoka Uingereza. Hi ni kitabu ambacho kimewapa motisha vizazi vya waandishi kwa miaka mingi nchini Nigeria, kote Afrika na kote duniani.

A Grain of Wheat cha Ngugi wa Thiong'o

A Grain of Wheat na Ngugi wa Thiong'o

Chanzo cha picha, Hisani

Maelezo ya picha, A Grain of Wheat na Ngugi wa Thiong'o

Kitabu hiki kinaangazia masuala kadha hadi wakati wa kupatikana uhuru wa Kenya na hadithi kuhusu masuala yaliyofuatia pamoja na ushawishi wa historia kwenye maisha ya watu na mahusiano.

Long Walk to Freedom cha Nelson Mandela

Long Walk to Freedom na Nelson Mandela

Chanzo cha picha, Hisani

Maelezo ya picha, Long Walk to Freedom na Nelson Mandela

Maisha ya Mandela yalikuwa moja ya hadithi bora zaidi katika karne ya 20. Hadithi hii inaangazia maisha ya Mandela akiwa kijana kwenye kijiji kidogo, hadi miaka yake ya mapindzui, hadi miaka mingi ya kufungwa na kuwa rais wa kupatanisha na mtu aliyeheshimiwa duniani. Muhimu kwa mtu ambaye anataka kuelewa historia.

Americanah cha Chimamanda Ngozi Adichie

Americanah na Chimamanda Ngozi Adichie

Chanzo cha picha, Hisani

Maelezo ya picha, Americanah na Chimamanda Ngozi Adichie

Kutoka kwa mmoja wa waandishi bora zaidi duniani inakuja hadithi ya raia wawili wa Nigeria wanaoelekea nchini Marekani na Uingereza na kuzua masuala kuhusu rangi, maisha ya waafrika ughabuni na kutafuta kutambuliwa na makao.

The Return cha Hisham Matar

The Return na Hisham Matar

Chanzo cha picha, Hisani

Maelezo ya picha, The Return na Hisham Matar

Kitabu kilichoandikwa kwa ustadi kinachoweka kwenye uzani masuala ya historia ya sasa nchini Libya huku mwandishi akiwa katika mikakati ya kumtafuta baba yake ambaye alitoweka kwenye jela za Gadhafi.

The World As It Is cha Ben Rhodes

Ni kweli kuwa Ben hana damu ya kiafrika. Lakini ni watu wachache wanaweza kuona dunia jinsi anavyoiona. Obama anasema amekuwa na kitabu cha Ben tangu kampeni yake yake ya kwanza ya kuwania urais. Obama amesema kuwa kimemfunza kuhusu jinsi ya kushughulikia sera za kigeni akiongeza kuwa ni moja ya hadithi amesoma kuhusu kuwatumikia watu kwa Marekani miaka minane Ikulu kama Rais.