Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vitabu ambavyo Obama angependa usome kwa sasa vilivyoandikwa na Waafrika
Wiki hii ninasafiri kwenda Afrika kwa mara ya kwanza tangu nitoke ofisini, bara la mambo mazuri, tamaduni nzuri na hadithi za kupendeza, Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Facebook.
Kwa miaka iliyopita nimevutiwa na fasihi isiyo ya kawaida kutoka nchi za Afrika. Ninapojiandaa kwa safari hii ningependa kutangaza vitabu ambavyo unaweza kuvisoma msimu huu wa joto vikiwemo kutoka kwa waandishi bora zaidi wa Afrika, aliandika Obama.
Vitabu hivyo ni vifuatavyo:
Things Fall Apart cha Chinua Achebe
Kitabu hiki kinatoa picha ya jamii ya kitamaduni inayopambana na kuwasili kwa mambo ya kigeni kutoka kwa wamishenari wa kikiristo hadi kwa wakoloni kutoka Uingereza. Hi ni kitabu ambacho kimewapa motisha vizazi vya waandishi kwa miaka mingi nchini Nigeria, kote Afrika na kote duniani.
A Grain of Wheat cha Ngugi wa Thiong'o
Kitabu hiki kinaangazia masuala kadha hadi wakati wa kupatikana uhuru wa Kenya na hadithi kuhusu masuala yaliyofuatia pamoja na ushawishi wa historia kwenye maisha ya watu na mahusiano.
Long Walk to Freedom cha Nelson Mandela
Maisha ya Mandela yalikuwa moja ya hadithi bora zaidi katika karne ya 20. Hadithi hii inaangazia maisha ya Mandela akiwa kijana kwenye kijiji kidogo, hadi miaka yake ya mapindzui, hadi miaka mingi ya kufungwa na kuwa rais wa kupatanisha na mtu aliyeheshimiwa duniani. Muhimu kwa mtu ambaye anataka kuelewa historia.
Americanah cha Chimamanda Ngozi Adichie
Kutoka kwa mmoja wa waandishi bora zaidi duniani inakuja hadithi ya raia wawili wa Nigeria wanaoelekea nchini Marekani na Uingereza na kuzua masuala kuhusu rangi, maisha ya waafrika ughabuni na kutafuta kutambuliwa na makao.
The Return cha Hisham Matar
Kitabu kilichoandikwa kwa ustadi kinachoweka kwenye uzani masuala ya historia ya sasa nchini Libya huku mwandishi akiwa katika mikakati ya kumtafuta baba yake ambaye alitoweka kwenye jela za Gadhafi.
The World As It Is cha Ben Rhodes
Ni kweli kuwa Ben hana damu ya kiafrika. Lakini ni watu wachache wanaweza kuona dunia jinsi anavyoiona. Obama anasema amekuwa na kitabu cha Ben tangu kampeni yake yake ya kwanza ya kuwania urais. Obama amesema kuwa kimemfunza kuhusu jinsi ya kushughulikia sera za kigeni akiongeza kuwa ni moja ya hadithi amesoma kuhusu kuwatumikia watu kwa Marekani miaka minane Ikulu kama Rais.