Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini unafaa kufanyisha mifupa mazoezi na manufa yake unapozeeka
Wengi wetu tuna kwepa kufanya mazoezi kwaajili ya kutupatia misuli na mifupa imara, linasema Shirika la Afya ya Umma Uingereza.
Shirika hilo limetoa ripoti mpya inayotoa ushauri kwa watu namna ya kuzeeka vizuri kwa kufanya mazoezi sahihi.
Wakati ujumbe kuhusu kufanya mazoezi ya kutikisa mwili kwa afya ya moyo na mapafu ukiwafikia watu, bado wengi wanauelewa mdogo kuhusu haja ya kuangalia uwezo wao pia.
Tunatakiwa kufanya mazoezi ya kutupa nguvu walau mara mbili kwa wiki.
Kunyanyua vitu vizito ni chaguo la kwanza, lakini kucheza muziki au tenisi inaleta matokeo mazuri pia, Kinasema kituo cha kuzeeka vizuri.
Shughuli zinazo faida zaidi ni:
•Kucheza mpira
•Kucheza Muziki
•Mazoezi ya kuzuia vitu (kusukuma au kuvuta vitu vizito
Kufanya Yoga na kuendesha baiskeli ni baadhi ya mazoezi mazuri kwaajili ya kuongeza nguvu ya misuli na mifupa pia kupata balansi.
Ni mwanaume mmoja tu kati ya wanaume watatu na mwanamke mmoja kati ya wanawake wanne wanafanya mazoezi sahihi na ya kutosha ili kuwa na afya njema lakini pia kuwa na nguvu za kutosha, wataalamu wanasema.
Kuimarisha misuli na mfupa lakini pia kufanya shughuli za kuleta usawa husaidia kuboresha mwili na kuleta ustawi katika umri wowote, na hupunguza hatari ya vifo vya mapema.
Lakini pia husaidia kuboresha Afya katika vipindi vigumu au kipindi maisha yanabadilika mfano wakati wa mimba, kipindi cha ukomo wa uzazi, mtu anapo ugua, wakati wa kustaafu na hata baada ya kupona ugonjwa.
Tumia au Poteza
Wataalamu wanawashauri vijana kujenga molekuli za misuli na mifupa, ambayo hufika kilele tunapo fikia miaka 30.
Watu wazima wanahitaji mazoezi ya kudumisha walicho kipata tayari na kupunguza kupungua asili kwa meolekuli kunako endana na umri.
Wale ambao ni dhaifu na wapo katika hatari ya kujeruhi mifupa, ikiwa ni pamoja na watu wenye tatizo la kusagika kwa mifupa, wanapaswa kuwa makini, hasa kwa shughuli kali kama vile tenisi, na kutafuta ushauri kutoka kwa daktari wao.
Dkt Zoe Williams kutoka shirika la afya ya uma Uingereza alisema: "Kuwa na nguvu si tu kuwa na mapigo ya moyo, ingawa hii ni njia nzuri ya kuanza. Shughuli za kuongeza nguvu na usawa zinashirikiana na shughuli za viungo kama kutembea na inaleta faida nyingi katika maisha yao. Wala hujachelewa kuanza"
Watu wazima wanapaswa kufanya:
•Angalau dakika 150 za mazoezi ya kawaida ya kutikisa mwili kama vile kutembea katika vihunzi kila wiki.
• Kufanya mazoezi ya kuongeza Nguvu kwa siku mbili au zaidi kwa wiki ili kufanyisha kazi misuli yote