Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jitihada za kutafuta mabaki ya marubani wa Marekani wa Vita vya Pili vya Dunia
Wapiga mbizi kutoka jeshi la wanamaji wa Ufaransa wanashirikiana na shirika moja la Marekani wa kutafuta mabaki ya marubani wawili wa Marekani wa vita vya pili vya Dunia mashariki pwani mwa kisiwa cha Ufaransa cha Corsica.
Shirika la (DPAA) limekuwa likisaidiwa na jeshi la Ufaransa kutafuta mabaki ya ndege.
Uchunguzi wa DNA kwa mabaki yaliyogunduliwa utasaidia kutambua marubani wa Marekani ambao wameorodheshwa kuwa waliotoweka wakiwa vitani.
Picha hizi zinaonyesha wapiga mbizi wa jeshi la Ufaransa kutoka FS Pluton M622 wakiogelea juu ya mabaki ya USAAF P-47 Thunderbolt ambayo ilianguka mwaka 1944.
Lengo la DPAA ni kuwatafuta wamarekani kutoka kwa mizozo iliyopita kuanzia Vita vya Pili vya Dunia.
Wapiga mbizi wafaransa na DPAA pia walikusanya mabaki kutoka kwa ndege kuyachunguza.
.