Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chumba cha ibada cha kanisa la Newport chanusurika moto mkali
Mhubiri wa kanisa lililochomeka amesema kuwa ni kitu cha kushangaza kwamba chumba cha ibada kilinusurika moto huo.
Kanisa hilo la jamii lenye umri wa miaka 130 la Bethel Community Church mjini Newport liliharibika kabisa baada ya moto kusambaa kutoka klabu ya burudani ya usiku.
Baadhi ya waumini walidai kwamba moto mtakatifu ulikilinda chumba hicho , kulingana na mhubiri Andrew Cleverly .
Bwana Cleverly pia anatumai kuokoa kanda za hotuba za marehemu babake ambazo huhifadhiwa katika chumba hicho.
Takriban wazimamoto 95 na polisi walifika tarehe 15 Juni lakini ilichukua hadi jioni ya siku iilyofuatia kuuzima moto huo.
Mwanamume mmoja wa miaka 43 na mwanamke mwenye miaka 36 walikamatwa kwa kushukiwa kuanzisha moto huo lakini wameachiliwa huku uchunguzi ukiendelea.
Picha kutoka ndani ya kanisa hilo inaonyesha kuwa kuna chumba kimoja ambacho hakikuchomeka.
Bw Cleverly anasema kuwa baadhi ya watu wa jamii waliamua kuwa kutokana na chumba hicho kutumika kwa maombi ndiyo sababu hakikuchomeka.
Watu wanadai kuwa sababu iliyochangia chumba hicho kukosa kuchomeka ni kuwa kulikuwa na moto wa kiroho ambao moto wa kawaida haungepenya.
Bw Cleverly ambaye baba yake alikuwa mhubiri wa kanisa ambaye alifariki miezi 18 iliyopita, alisema chumba hicho ndimo kanda za video za mahubiri ya baba yake zilikuwa zinahifadhiwa.
"Wakati itakuwa salama, ningependa kujaribu kutoa kanda hizo," alisema.
Pia alishukuru jamii na wafanyabiashara kwa kulisaidia kanisa hilo.