Chumba cha ibada cha kanisa la Newport chanusurika moto mkali

On the left, a fire engulfs Bethel Community Church. On the right, the prayer room and its furniture survived relatively unscathed.

Chanzo cha picha, Andy Wright/Bethel Community Church

Maelezo ya picha, Bw Cleverly anasema kuwa baadhi ya watu wa jamii waliamua kuwa kutokana na chumba hicho kutumika kwa maombi ndiyo sababu hakikuchomeka.

Mhubiri wa kanisa lililochomeka amesema kuwa ni kitu cha kushangaza kwamba chumba cha ibada kilinusurika moto huo.

Kanisa hilo la jamii lenye umri wa miaka 130 la Bethel Community Church mjini Newport liliharibika kabisa baada ya moto kusambaa kutoka klabu ya burudani ya usiku.

Baadhi ya waumini walidai kwamba moto mtakatifu ulikilinda chumba hicho , kulingana na mhubiri Andrew Cleverly .

Bwana Cleverly pia anatumai kuokoa kanda za hotuba za marehemu babake ambazo huhifadhiwa katika chumba hicho.

Takriban wazimamoto 95 na polisi walifika tarehe 15 Juni lakini ilichukua hadi jioni ya siku iilyofuatia kuuzima moto huo.

Pastor Andrew Cleverly
Maelezo ya picha, Bw Cleverly anasema kuwa baadhi ya watu wa jamii waliamua kuwa kutokana na chumba hicho kutumika kwa maombi ndiyo sababu hakikuchomeka.

Mwanamume mmoja wa miaka 43 na mwanamke mwenye miaka 36 walikamatwa kwa kushukiwa kuanzisha moto huo lakini wameachiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

Picha kutoka ndani ya kanisa hilo inaonyesha kuwa kuna chumba kimoja ambacho hakikuchomeka.

Bw Cleverly anasema kuwa baadhi ya watu wa jamii waliamua kuwa kutokana na chumba hicho kutumika kwa maombi ndiyo sababu hakikuchomeka.

Watu wanadai kuwa sababu iliyochangia chumba hicho kukosa kuchomeka ni kuwa kulikuwa na moto wa kiroho ambao moto wa kawaida haungepenya.

Bethel Community Church in Newport on fire

Chanzo cha picha, Katie Maddocks

Maelezo ya picha, Watu wanadai kuwa sababu iliyochangia chumba hicho kukosa kuchomeka ni kuwa kulikuwa na moto wa kiroho ambao moto wa kawaida haungepenya.

Bw Cleverly ambaye baba yake alikuwa mhubiri wa kanisa ambaye alifariki miezi 18 iliyopita, alisema chumba hicho ndimo kanda za video za mahubiri ya baba yake zilikuwa zinahifadhiwa.

"Wakati itakuwa salama, ningependa kujaribu kutoa kanda hizo," alisema.

Pia alishukuru jamii na wafanyabiashara kwa kulisaidia kanisa hilo.

Havelock Street Presbyterian Church, Newport.

Chanzo cha picha, Jagger/Geograph

Maelezo ya picha, Pia alishukuru jamii na wafanyabiashara kwa kulisaidia kanisa hilo.