Mourinho: Naibu wangu anaweza kuisaidia Arsenal

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atamsaidia naibu kocha wake Rui Faria kufungasha virago iwapo Arsenal wanamtaka kuwa mkufunzi wao mpya.
Imeripotiwa kuwa Faria mwenye umri wa miaka 42 ameorodheshwa na Arsenal miongoni mwa makocha wapya wanaotarajiwa kurithi kazi ya Arsene Wenger katika uwanja wa Emirate.
Faria amekuwa naibu wa Mourinho katika klabu sita tangu walipokuwatana katika klabu ya Porto miaka 14 iliopita na kusaidia kushinda matajai 25.
Mourinho amesema kuwa naibiu wake atakuwa kocha mzuri kujaza pengo hilo wakati Wenger atakapoondoka baada ya kipindi cha miaka 22.
Ninasema hivyo kwasababu ni naibu wangu na rafiki yangu, alisema raia huyo wa Ureno.Iwapo rafiki yangu siku moja ana uwezekano wa kuwa mkufunzi mkuu nitamsaidia kufungayna virago na kuondoka na kumtakia kila la heri.
Nilikutana naye alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu na tukafanya kazi pamoja kwa miaka 18 .Ni rafiki yangu mkuu zaidi ya naibu kocha. Iwapo muda wake wa kuondoka utafika nitafurahia.
Naibu kocha wa liverpool Zeljko Buvac ia amepenmekezwa kumrithi Arsene Wenger -kwa sasa raia huyo wa Ujerumani amechukua likizo katika klabu hiyo ya Mersyside kwa sababu zake za kibinafsi.
Wachezaji wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta na Patrick Vieira pia wametajwa mbali na aliykuwa kocha wa Barcelona Luis Enrique na mwnzake wa Juventus Massimiliano Allegri pia wametajwa.












