Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi: Madai ya kutekelezwa kwa mashambulizi ya kemikali ni 'hila'
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov amesema kuwa ripoti kuhusu shambulio la silaha za kemikali ni njama za washirika wa nje.
Marekani na Ufaransa zimesema kuwa zina ushahidi kuwa shambulio lilitekelezwa, wakiungana na Uingereza, wanafikiria kutekeleza mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria.
Urusi, mshirika wa Syria, imeitahadharisha Marekani kuwa mashambulizi ya anga yanaweza kusababisha vita mpya.
Wataalam huria wa maswala ya silaha za kemikali wako njiani kuelekea Ghouta kutafuta ushahidi .Wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi.
Wito wa kuchukuliwa hatua umekuja baada ya kinachoshukiwa kuwa shambulio la kemikali kutokea mjini Douma mashariki mwa Ghouta siku ya Jumamosi, shambulio lililogharimu maisha ya watu kadhaa, kwa mujibu wa wanaharakati wa upinzani, waokoaji na matabibu.
Mashambulizi ya kemikali yanadaiwa kutokea nchini Syria hapo kabla.Mwaka jana, Marekani ilianzisha mashambulizi ya kulipa kisasi moja likielezwa kutokea mjini Khan Sheikhoun.
Serikali ya Rais Bashar Al Assad ambayo inaungwa mkono na Urusi imekana kuhusika na shambulio lolote la kemikali, ikisema ripoti hizo ni za 'kutunga'.
Baada ya majuma sita ya mapambano na vifo vya raia takriban 1,700 mashariki mwa mji wa Ghouta, serikali ya Sria sasa inadhibiti eneo hilo,lililo nje ya Damascus.
Zoezi la kuondoa kundi la mwisho la watu 4000 la wapiganaji wa kiislamu na raia limeendelea Ijumaa, kwa mujibu wa waangalizi wa haki za binadamu.