Nini hasa kilichotokea baada ya kuchukuliwa kwa picha hizi

Mwanahabari wa picha Eddie Adams alichukua moja ya picha maarifu zaidi za vita vya Vietnam - wakati tukio la mauaji yaliyotokea wakati wa ghasia za uasi wa Tet . Ilimpatia umaarufu katika maisha yake, lakini pia ilimpatia huzuni.

Onyo: taarifa hii inajumuisha picha ya Adam ya wakati wa ufyatuaji risasi, na maelezo yake ya lugha ya kutisha.

Risasi aina ya bastola tayari imeelekezwa kwenye mkono wa mwanamume mmoja huku uso wa mfungwa kinaonekana kupinda kutokana na msukumo wa risasi inayoingia kwenye fuvu la kichwa chake.

Upande wa kushoto wa dirisha, askari anayetazama tukio anaonekana kupatwa na mshtuko .

Ni vigumu kutopatwa na hisia za hasira na majuto, kwa mtu anayefahamu kuwa kile anachokishuhudia ni wakati wa mtu kukata roho.

Wataalam wa vilipuzi wanasema picha - ambayo ilikuja kufahamika kama mauaji ya Saigon - Saigon Execution - inaonesha risasi ikiingia ndani ya kichwa cha mwanaume kwa sekunde chache .

Picha ya Eddie Adams ya Brigadier General Nguyen Ngoc Loan akimpiga risasi mfungwa katika gereza la Cong nchini Vietnum, inachukuliwa kama moja ya picha zilizo na ushawishi mkubwa katika vita vya Vietnam.

Wakati huo, picha hiyo ilichapishwa tena kote duniani na ikawa kielelezo kwa wengi cha ukatili uliofanyika katika vita hivyo.

Picha hiyo pia ilichochea kuenea kwa hisia nchini Marekani kwamba vita hivyo havikuwa na maana - na kwamba Marekani isingeshinda vita.

"Kuna kitu fulani kuhusu muundo wa picha ambacho huwaathiri sana watazamaji na kubakia ndani ya hisia zao," anasema Ben Wright, mkurugenzi msaidizi wa mawasiliano katika kituo cha Dolph Briscoe cha masuala ya Historia ya Marekani.

Kituo hicho chenye makao yake katika Chuo Kikuu cha Texas kimehifadhi picha za Adams, nyaraka na mawasiliano.

"Picha za filamu za ufyatuaji risasi, hazina hali ya dharura na maafa kama ilivyokuwa awali."

Lakini hazijafanya hivyo, hazikuweza kuelezea kikamilifu mazingira halisi katika mitaa ya Saigon tarehe 1 Februari 1968, siku mbili baada ya vikosi vya Vietnum - People's Army of Vietnam na Viet Cong kuanzisha uasi katika mwaka mpya wa Vietnum. Makumi kadhaa ya miji ya kusini mwa Vietnam yalijipata ghafla kwenye vita hivyo.

Mapigano makali ya mitaa yalikuwa yameitumbukiza Saigon katika ghasia wakati jeshi la kusini mwa Vietnam yalipomkamata kiongozi wa kikosi cha Viet Cong , Nguyen Van Lem, kwenye eneo la makaburi ya pamoja ya raia 30.

Adams alianza kuchukua picha wakati Lem alipoanza kuzunguka kwenye mitaa juu ya gari la Loan ina ya Jeep.

Loan alisimama kando ya Lem kabla ya kuelekeza bastola yake kwenye kichwa cha mfungwa.

"Nilidhani alienda kumtishia jamaa yule," Alikumbuka Adams, "kwa hiyo nikanyenyua tu kawaida kamera yangu na kuchukua picha ."

Lem anaaminiwa kuwa alimuuua mke na watoto sita wa mmoja wa rafiki zake Loan. Alifyatua bastola yake.

"Kama unasita, kama hukuwa unafanya kazi yako, wasingekufuata," jenerali alielezea juu ya masikitiko ya vitendo vyake.

Loan alikuwa na jukumu muhimu katika saa 72 za mwaka wa uasi wa Vietnum, ya kuchochea majeshi kuzuia kuanguka kwa Saigon, kwa mujibu wa Colonel Tullius Acampora, ambae alifanya kazi kwa miaka miwili kama ofisa wa jeshi la Marekani wa mawasiliano wa Loan.

Adams alisema kuwa mtazamo wake wa moja kwa moja ulikuwa kwamba Loan alikuwa mtu "asiye na huruma, na muuaji ". Lakini baada ya kusafiri nae katika maeneo mbali mbali ya Vietnum alibadili mtazamo wake kumhusu.

"Matendo yake yalitokana na Vietnam ya wakati huo na nyakati zake," alisema Adams katika taarifa yake fupi kutoka Vietnam.

Mnamo mwezi Mei mwaka uliofuatia, picha yake ilimpatia Adams tuzo ya Pulitzer ya mpiga picha aliyepata picha bora ya tukio.

Lakini licha ya tunu hili la mafanikio makubwa ya mwanahabari na barua za pongezi kutoka kwa washindi wengine wa tuzo ya Pulitzer, Rais Richard Nixon na hata watoto wa shule kote nchini Marekani, picha hio ilimfanya Adams ajihisi mwenye majuto.

"Nilipata pesa kwa kumuonesha mtu mmoja akimuua mwingine," Adams alisema katika sherehe nyingine ya tuzo iliyofanyika baadae . "Maisha mawili yaliangamizwa, na nilikua ninalipwa kwa hilo. Nilikuwa shujaa."

Adams ana Loan waliendelea kuwasiliana, na hata wakawa marafiki baada ya jenerali huyo kutorokea Vietnum Kusini mwishoni mwa vita dhidi ya Marekani.

Lakini wakati Loan alipowasili, idara ya uhamiaji ya Marekani ilitaka kumrejesha Vietnum, hatua iliyochangiwa na picha. Walimuendea Adams atoe ushahidi dhidi ya Loan, lakini badala yake Adams alitoa ushahidi uliomtetea.

Hata Adams akaonekana kwenye televisheni akielezea mazingira aliyochukulia picha hiyo.

Hatimae baraza la Congress liliondoa amri ya kumrejesha nyumbani na Loan karuhusiwa kubaki, akafungua mgahawa kwenye kitongoji kimoja mjini Washington, DC, unaotoa huduma ya mikate aina ya hamburgers, pizza na vyakula vya asili ya Vietnam.

Makala ya gazeti kuu la Washington Post inaonesha picha ya mwanaume kikongwe aliyekaa mbele ya mgahawa akitabasamu.

Lakini hatimae alilazimishwa kustaafu baada ya taarifa kuhusu maisha yake ya nyuma zilipoharibu biashara yake. Adams alikumbuka kwamba katika ziara yake ya mwisho katika mgahawa huo alipata maandishi ya matusi kumhusu Loan yaliyoandikwa chooni.

Mhariri wa picha ya Adams katika shirika la habari la AP, Hal Buell, anasema kuwa mauaji ya Saigon bado yanakumbukwa miaka 50 baadae kwa sababu ya picha "katika fremu moja, iliyo kama ishara ya ukatili mzima uliofanywa wakati wa vita vya Vietnum".

"Kama ilivyo kwa kitu chochote cha mfano, inaelezea kwa kifupi kilichofanyika kabla, kuonesha wakati wa sasa na kama ukiangalia kwa umakini wa kutosha, inatuelezea kitu kuhusu hali ya baadae ya ukatili wa vita "

Na Buell anasema kuwa uzoefu wa kazi hiyo ulimfundisha Adams kuhusu vikomo vya picha moja katika kuelezea taarifa nzima.

"Eddi amenukuliwa akisema kiwa upigaji picha ni silaha yenye nguvu ,"Buell anasema . "Kwa asili upigaji picha unachagua . Huchukua tukio la wakati mmoja , kulitenganisha na nyakati za awali na baada ya hapo huenda ukapelekea kubadilika kwa maana yake."

Adams aliendelea kupanua taaluma yake, na kushinda zaidi ya tuzo 500 za uanahabari wa picha na upigaji picha ambapo miongoni mwa watu wa kuheshimika miongoni mwao Ronald Reagan, Fidel Castro na Malcolm X.

Lakini licha ya mafanikio yote hayo baada ya Vietnam, picha yake maarufu itabakia kuwa na Adams.

"Watu wawili walikufa katika picha hiyo" Adams aliandika kufuatia kifo cha Loan kilichotokana na maradhi ya saratani mnamo mwaka 1998. "Generali huyo aliwaua wafungwa wa gereza la Vietnum la Cong; Nilimuua jenerali na kamera yangu."

.