Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanajeshi mwengine wa Korea Kaskazini ahamia Korea Kusini
Jeshi la Korea Kusini limetoa onyo la kuwafytaulia risasi wanajeshi wa Korea Kaskazini wanaomtafuta mwanajeshi aliyeihama nchi yao.
Mwanajeshi wa Korea Kaskazini alikuwa amevuka katika eneo lenye ulinzi mkali wa kijeshi muda mfupi baada ya 23:00 GMT siku ya Jumatano.
Alionekana kwenye ukungu mkubwa katika kituo cha ukaguzi, amesema mwanajeshi wa Korea Kusini.
Mwanajeshi huyo ni wa nne wa Korea Kaskazini kuihama nchi hiyo mwaka huu.
Kisa hiki kimetokea wiki kadhaa baada ya kisa cha kuchekesha cha hivi majuzi.
Kisa hicho cha tarehe 13 mwezi Novemba, mwanajeshi wa Korea Ksakzini alipigwa risasi alipokuwa akivuka kuelekea kusini mwa kijiji cha Panmunjom.
Tukio hilo la Alhamisi lilitokea katika kituo cha ukaguzi, amesema Roh Jae-cheon, msemaji wa Korea Kusini wa muungano wa machifu.
Bw Roh aliongeza mwanajeshi huyo alikamatwa na ''akahifadhiwa vizuri''. Maafisa wanachunguza sababu ya yeye kujaribu kuvuka mpaka.
Mwanajeshi huyo anayekisiwa kuwa na miaka 19, alikuwa amebeba bunduki aina ya AK-47.
Hakuna ufyatulianaji wa risasi ulishuhudiwa wakati huo.
Lakini muda mfupi baada ya mwanajeshi huyo kuvuka , kundi la walinzi waliokuwa wakiulinda mpaka kutoka Kaskazini waliwasili kumtafuta mwenzao, kulingana na wizari ya usalama ya Korea Kusini.
Wanajeshi wa Korea Kusini walimimina risasi 20 za kutoa tahadhari.
Maafisa wamesema sauti hiyo ya milio ya risasi kutoka kaskazini ilisikika dakika 40 baadaye, lakini hakuna risasi zilizopatikana kuvuka mpaka.