Uchaguzi Ujerumani: Merkel awania muhula wa nne

Mamilioni ya watu nchini Ujerumani wanapiga kura ambapo chanselal Angela Merkel anatarajiwi kupata ushindi.

Anawania muhula wake wa nne kuendelea kuuweka mungano wa CDU/CSU kuwa mkubwa zaidi bungeni.

Mshirika wake chama cha SPD ndiye mpinzani mkuwa huku chama cha mrengo wa kulia cha AfD kikitarajwa kupata viti vyake vya kwanza bungeni.

Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura inaratajiwa kuwa ya juu.

Hadi mchana watu wengi walikuwa wamepigakura katika maeneo mengi kuliko wakati kama huo miaka minne iliyopita.

Bi Merkrel alipiga kura yake huko Berlin huku mgombea wa SPD wa wadhifa wa chansela Martin Schulz, akipiga kura yake katika mji wa Wuerselen magharibi mwa Ujerumani.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mwendo saa mbili asubuhi saa za Ujerumani na vinatarajiwa kufungwa sa kumbi na mbili alasiri na matokeoa ya kwanza yanatarajiwa muda mfupi baaadaye.