Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watawa bandia wajaribu kuiba kwenye benki Marekani
Maafisa wa uchunguzi wa jinai nchini Marekani, FBI, wanawatafuta wanawake wawili ambao walijaribu kuiba pesa kutoka kwenye benki moja jimbo la Pennsylvania wakiwa wamevalia kama watawa.
Mmoja wa wanawake hao alichomoa bunduki na kuwaamrisha makarani wampe pesa wakati wa kisa hicho katika mji wa Tannersville.
Wote wawili walikuwa wamevalia mavazi ya watawa na mmoja alikuwa amevalia miwani.
Wanadaiwa kukimbia na kutoroka baada ya mmoja wa makarani wa benki kufungulia king'ora.