Dubu amng'ata mgeni kwenye mbuga ya wanyamapori China

Chanzo cha picha, Weibo/Mr Chen
Dubu amemng'ata mgeni kwenye mbuga ya wanyama pori ncjini China sehemu ambayo mwanamke alifarikia dunia baada ya kushambuliwa na dubu mwaka uliopita
Mwanamume huyo alikuwa amepuuza onyo na kuteremsha kioo cha gari lake kuwalisha dubu katika mbuga ya Badaling karibu na mji wa Beijing.
Alinusurika na majeraha madogo.
Tangu wakati huo mamlaka zimeamrisha mbuga hiyo kuboresha hatua za kiusalama ikiwemo kupunguza idadi ya wageni.
Mwaka uliopita mwanamume mmoja na mama yake walitoka ndana ya gari lao ambapo walishambuliwa na duma. Mama alikufa muda baadaye.

Chanzo cha picha, Weibo/Mr Chen
Katika kisahiki cha siku Ijumaa mwanamme kwa jina Chen, alikuwa akiendesha gari ndani ya mbuga hiyo akiwa na rafiki yake.
Licha ya onyo, wanaume hao waliamua kuteremsha vyoo vya gari lao na kujaribu kuwarushia dubu chakula.
Dubu mmoja alipanda kwenye mlango wa gari na wakati Chen alijaribu kupandisha kio kikakumbwa na hitilabu na badala yake kikaanza kuteremka, ndipo yule dubu akamgata kwenye bega lake.

Chanzo cha picha, Getty Images












