Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump aelezea mipango yake juu ya Afghanistan
Rais Donald Trump ameelezea mpango wake kuhusiana na Afghanstan na ukanda wa Asia ya kusini.
Amesema pia kuwa anaongeza idadi ya wanajeshi watakao pelekwa nchini Afghanstan.
Akizungumza kupitia Televishen, Rais Trump amesisitiza kuwa kipaumbele cha Marekani ni kutekeleza masuala yenye maslahi katika usalama wa taifa hilo, kutokomeza mtandao wa ugaidi.
Amesisitiza pia kuwa kitendo cha Marekani kujiondoa kwa haraka Afghanistan, kitatatoa mwanya kwa ugaidi kujiimarisha zaidi kama ilivyotokea Iraq.
Hata hivyo Trump amekwepa kuzungumzia moja kwa moja muda wa mwisho wa ushiriki wa Marekani nchini Afghastan na idadi kamili ya ongezeko la wanajeshi.
Rais Trump ameitupia lawama Pakistan kwa madai kuwa inawahifadhi magaidi ambapo amesema suala hilo linapaswa kuachwa mara moja.
Katika hatua nyingine amezungumzia mpango wa Marekani kuimarisha mpango wa ushirikiano na India.