Manowari ya jeshi la Marekani, USS Indianapolis, iliyozama miaka 72 iliyopita yapatikana

This 1937 image released by the US Navy shows the Portland-class heavy cruiser USS Indianapolis in Pearl Harbour in 1937

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, USS Indianapolis - picha ya mwaka 1937

Manowari ya jeshi la Marekani ya USS Indianapolis ambayo ilizama wakati wa vita vya pili vya dunia, imepatikana kwenye bahari ya Pacific, Miaka 72 baada ya kuzamishwa na nyambizi wa Japan.

USS Indianapolis ilikuwa ikirejea kutoka oparesheni ya siri ya kupeleka sehemu za kunda bomu la atomic ambalo baadaye lilitumiwa huko Hiroshima.

Manowari hiyo ilipatikana kilomita 5.5 chini ya bahari.

Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Paul Allen, ambaye aliongoza kikosi cha kutafuta manowari hiyo alisema ugunduzi huo ni wa kutia moyo.

USS Indianapolis iliharibiwa tarehe 30 Julai mwaka 1945 katika habari ya Ufilipino kati ya Guam na Leyte baada ya kugongwa na kombora kutoka kwa nyambizi ya Japan.

A handout photo made available on 19 August 2017 courtesy of Paul G. Allen shows an image shot from a remotely operated vehicle showing what appears to be the painted hull number "35."

Chanzo cha picha, Paul G Allen

Maelezo ya picha, Picha ya Indianapolis baharini

Kilikuwa kisa kibaya zaidi cha kupotea kwa maisha kulikumba jeshi la wanamaji wa Marekani.

Kulikuwa na wanajeshi 1,196 ndani ya manowari hiyo na ni kati ya wanajeshi 800 na 900 walinusurika kuzama.

Lakini manowari hiyo haikutuma ishara na hadi wakati masura walipatikana siku nne baadaye ni watu 316 tu waliopatikana wakiwa hai katika eneo hilo lenye papa wengi.

Meli hiyo ni maarufu kwa kufanya safari ya siri ya kusafiirjha sehemu za kuunda bomu la atomic lilifahamika kama "Little Boy" .

A steel part showing the the text: USS Indianapolis, spare parts

Chanzo cha picha, Paul G Allen

Maelezo ya picha, Sehemu za USS Indianapolis

Bidhaa hizo zilipelekwa katika kisiwa cha Tinian kwenye kambi ya jeshi la Marekani ambayo ilifanya shambulizi la kwanza na bomu la nyuklia.

Siku nne baadaye Indianapolis ilizama chini ya wiki moja kabla ya bomu hilo la nyuklia ililosaidia kuunda kuharibu mji wa Hiroshima.

Sawa na bomu lenye jina "Fat Man" lililoangushwa mji wa Nagasaki, ambalo liliilazimisha Japan kuachana na vita na kumalizika kwa vita vya pili vya Dunia.