Gari lawagonga wanajeshi wa Ufaransa mjini Paris 6 wajeruhiwa

Gari limegonga kundi la wanajeshi mjini Paris, Ufaransa na kuwajeruhi sita wawili vibaya.

Oparesheni ya dharura kwa sasa inaendelea kutafuta gari hilo na dereva aliyetekeleza kisa hicho katika mtaa wa Levallois-Perret.

Meya wa eneo hilo Patrick Balkany, alisema hana shaka kuwa kitendo hicho kilikuwa ni cha makusudi.

Ufaransa imekuwa chini ya hali ya tahadhari tangu mwezi Novemba mwaka 2015.

Tangu wakati huo zaidi ya watu 230 wameuliwa kwenye misururu ya mashambulizi ya kigaidi.

Hayo ni pamoja na mashambulizi dhidi ya vikosi vilivyojihami vikali vilivyotabakaa sehemu tofauti mjini.

Shambulizi hilo la siku ya Jumatano lilitokea karibu na ukumbi wa mji ulio mtaa wa Levallois-Perret.