Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watu kadhaa wajeruhiwa kwa risasi nje ya msikiti Ufaransa
Watu 8 wamejeruhiwa wakati wa ufytuajia risasi nje ya msikiti kusini mwa Ufaransa.
Waumini waliokuwa wakiondoka kwenye msikiti wa Arrahma, walikaribiwa na washukiwa wawili waliokuwa na bunduki ambao walifyatua risasi kwa umati.
Polisi wanasema kuwa hawachukulii kisa hicho kuwa cha kigaidi.
Watu wanne walijeruhiwa nje ya mskitini wanne wakiwa wa familia moja. akiwemo msichana ya miaka 7.
Wawili kati ya watu 8 waliojeriawa walilazwa hospitalini.
Walioshudia wanasema kuwa watu kadha karibu na msikiti walianza kukimbia wakati waliona washukiwa wawili wakiondoka kwenye magari yao na kuwakaribia wakiwa na bunduki mkononi.
Kisa cha Avigno hakichukuliwi kama cha kigaidi, ofisi mkuu wa mshataka ilisema.
Kwa sasa idara ya ujasusii inakifuatilia kisa hicho.