Mwana wa simba Cecil auwawa Zimbabwe

Chanzo cha picha, AFP PHOTO / ZIMBABWE NATIONAL PARKS
Miaka miwili baada ya simba Cecil kuuwawa na mwindaji nchini Zimbabwe na kuzua shutuma za kimataifa, mwanawe naye ameuwawa.
Xanda, simba mwenye umri wa miaka sita alipigwa risasi na mwindaji.
Anaripitiwa kufa nje ya mbuga ya Hwange kaskazini mwa Zimbabwe.
Simba huyo alikuwa amewekewa kifaa cha kumfuatilia na watafiti wa chuo cha Oxfiord.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa akiwa na umri wa miaka sita, Xanda alikuwa amefika umri wa kuweza kulengwa na wawindaji.
Wawindaji hawa, wenge kutoka Marekani, Uingereza na Afrika Kusini, hulipa maelfu ya pesa kuweza kuwinda, na fedha hizo hutumiwa kugharamia watu ambao huwalinda wanyamapori.
Haijulikani ni nani alikuwa amelipa ili kumuua Xanda.








