Gari la thamani kubwa la McLaren laharibiwa kabisa kwenye ajali

Chanzo cha picha, Trowbridge Fire Station
Gari la thamani kubwa aina la McLaren liliteketea moto kabisa baada ya kugonga nyumna na kushika moto.
Dereva na abiria wa gari hilo aina ya 570S ambalo thamani yake ni karibu pauni 143,000 walinusurika na majeraha madogo kufuatia ajali hiyo.

Chanzo cha picha, Trowbridge Fire Station
Wazima moto waliokuwa eneo la ajali walipata kuwa waliokuwa ndani ya gari walikuwa wametoka na kuliacha gari hilo likiteketea .
Haijulikani gari hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi gani.
Grai hilo linaweza kukimbia kwa kasi ya kuanzia sufuru hadi kilimita 100 kwa saa kwa sekunde 3.2 tu

Chanzo cha picha, Trowbridge Fire Station








