Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maelfu waandamana kudai haki za wapenzi wa jinsia moja Marekani
Maelfu ya watu wameandamana katika kile wanachokiita kudai haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja mjini Washington, nchini Marekani.
Yanatajwa kuwa maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa tokea kuingia madarakani kwa Trump.
Wengi wao wanadai kuwa wanapata vitisho na hawajui mustakabali juu ya maisha yao.
Lakini watetezi wa haki za binaadam wanasema bado wanatengwa katika masuala kama ajira.
Maandamano haya yamekuja karibia mwaka mmoja baada ya watu 49 kuuawa kwa kupigwa risasi kwenye klabu moja ya usiku ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.