Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanajeshi kukabiliana na maandamano Venezuela
Serikali ya Venezuela imesema ni muhimu kuwepo kwa vikosi vyake vya jeshi katika mji wa Tachira ulio karibu na mpaka wa Colombia.
Waziri wa ulinzi amesema zaidi ya wanajeshi elfu mbili watatumwa eneo hilo kukabiliana na maandamano yanayoendelea dhidi ya serikali.
Mapema wiki hii kijana wa miaka 15 aliuawa katika mji huo alipokuwa akinunua maua kwa ajili ya mama yake.
Kwa wiki hii pekee wameuawa watu watatu katika eneo hilo kutokana na maandamano yanayoendelea.
Kwa nchi nzima mpaka sasa wameuawa zaidi ya watu 43 kwa maandamano yaliyodumu chini ya miezi miwili.
Raia sita wa Colombia walikamatwa mjini Tachira kwa kudaiwa kuchochea maandamano hayo.