Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Clinton: Nalaumu FBI na wadukuzi wa Urusi
Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani Hillary Clinton amewalaumu wadukuzi wa Urusi na mkurugenzi wa Ujasusi nchini humo kwa kushindwa kwake katika uchaguzi mkuu uliopita
Aliambia mkutano mjini New York kwamba angeshinda kura hiyo iwapo uchaguzi huo ungefanyika tarehe 20 mwezi Oktoba kabla ya kuchapishwa kwa barua ya mkurugenzi wa FBI James Comey akilielezea bunge la seneti kwamba FBI imeanzisha uchunguzi kuhusu hatua yake ya kutumia barua pepe za binafsi.
Alisema kwamba alikuwa amefanya kampeni nzuri na akapoteza kutoka na maswala yaliofanyika katika kipindi cha siku kumi za mwisho.
Anasema kuwa sasa amerudia uanaharakati akisema hatua yake inalenga kuweka upinzani mkali dhidi ya rais Trump ambaye amemkosoa kwa sera zake za kigeni mbali na utumizi wake wa mtandao wa Twitter.