Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani kugharamia mtambo ya kujikinga Korea Kusini
Korea kusini inasema kuwa Marekani imekubali kulipa dola bilioni moja za kujenga kinga ya dhidi ya makombora ya Korea Kaskazini.
Awali rais Trump alikuwa amesema Korea kusini itagharamia ujenzi huo.
Maafikiano hayo yanajiri baada ya washauri wa maswala ya usalama wa mataifa hayo mawili kuzungumza kwa njia ya simu.
Ngao hiyo maalum ambayo inajengwa kwa sasa inalenga kudungua makombora yote yanayofyatuliwa kutoka Korea kaskazini.
Marekani imekubali kufadhili mradi huo kifedha huku korea kusini ikitakiwa kutoa ardhi.