Wakenya watawala mbio za London Marathon

Mary Keitany

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mary Keitany

Wakenya Mary Keitany na Daniel Wanjiru wameibuka washindi wa mbio za London Marathon.

Keitany ameandikisha rekodi mpya ya wanawake pekee katika mbio za nyika kwa muda wa 2:17:01.

Amechukua taji hilo kwa mara ya tatu sasa akiwa na miaka 35.

Muithiopia Tirunesh Diababa amemaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa 2:17:56

Katika mbio za wanaume Daniel Wajiru wa Kenya ameshinda kwa muda wa 2:05:56 na kufuatwa kwa karibu na Kenenisa Bekele wa Ethiopia

Kenenisa Bekele (kushoto) na Daniel Wanjiru
Maelezo ya picha, Kenenisa Bekele (kushoto) na Daniel Wanjiru