Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Muuaji aliyeonekana Facebook ajiua
Polisi nchini Marekani wamesema mtu ambaye alifanya mauaji kisha kutuma video ya mauaji hayo katika mtandao wa Facebook amejiua mwenyewe.
Wamesema Steve Stephens alijiua wakati maafisa wa polisi walipolikaribia Gari lake walipokuwa wakimkimbiza takribani kilomita 150 kutoka Cleveland, Ohio, eneo la mauaji yaliyofanyika jumapili.
Picha za video za babu akipigwa risasi zilisalia kwenye mitandao ya kijamii kwa saa mbili bila kuondolewa.
Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg, alieleza maskitiko yake kwa ndugu na akaahidi kuwa kampuni itafanya kila linalowezekana kuzuia jambo kama hilo kuwekwa tena mtandaoni.