Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wafanyikazi 4 wa misaada watekwa nyara Mogadishu
Wafanyi kazi wanne wa shirika la utoaji misaada nchini Somalia, wametekwa nyara katika eneo la Gedo, kaskazini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Wanne hao walikuwa wakifanya kazi na shirika la Afya Duniani WHO, katika mji wa Luq, kwenye kampeini ya kupambana na ugonjwa wa polio.
Duru zasema kuwa walitekwa na wanamgambo wa Al Shabaab, lakini taarifa hiyo bado hazijathibitishwa.
Eneo la Gedo, limeathirika pakubwa na ukame, na ni mojawapo ya maeneo ambayo wapiganaji wa al-Shabaab, wanadai kwamba wanawapa chakula cha msaada watu walioathirika na ukame huo.