Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Aliyeshambulia raia Urusi ana asili ya kutoka Kyrgyzstan
Mwanamume anayeshukiwa kuwaua watu 14 kwa kulipua treni ya St Petersburg ni mwenye asili ya kutoka Kyrgyzstan aliyepata uraia wa Urusi, idara ya usalama ya Asia ya kati imesema.
Vikosi vya usalama nchini Urusi wako kwenye taadhari kubwa baada ya kutokea
Watu 49 walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea kwenye vituo viwili vya treni ya chini ya ardhi mjini St Petersburg.
Maafisa wa Kyrgyz wamemtaja mshukiwa huyo kuwa Akbarzhon Jalilov, wa kabila la Uzbek aliyezaliwa Osh mnamo 1995.
Kuna taarifa zinazo kinzana kuhusu iwapo alikuwa mlipuaji wa kujitoa muhanga.
Awali vyombo vya habari vimeripoti vikinukuu vyanzo vya usalama vikisema milipuko hiyo huenda imelipuliwa na mtu aliyejitoa muhanga kutoka eneo la Asia ya Kati.
Kifaa kingine kilichokutwa kwenye stesheni nyingine kiliteguliwa na wataalam wa kutegua mabomu.
Wachunguzi nchini Urusi wamelichukulia tukio hilo kuwa ni shambulio la kigaidi.
Rais Vladmir Putin yuko St.Petersburg kupata maelezo ya wataalam wa masuala ya usalama, pia aliweka mashada ya maua kuwakumbuka walioathirika kwenye ajali hiyo, amesema ni mapema mno kujua chanzo cha tukio hilo lakini uchunguzi unafanyika.
''Sababu ya tukio hilo haijafahamika, hivyo ni mapema kuzungumzia kuhusu hilo.uchunguzi utaonyesha , lakini maelezo yote yatatizamwa, ilikupata sababu ya ajali hiyo na sababu ya uhalifu huo, juuu ya yote ugaidi, tutaona, uchunguzi utatupa majibu yote kuhusu kilichotokea.'' alieleza Putin