Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tamasha la kutatanisha lafungiwa nchini Urusi
Tamasha nchini Urusi la mpiga picha anyetatanisha wa marekani limefungwa baada kupingwa na wanaharakati.
Picha ziliyopigwa na Jock Sturges inajumuisha picha zinazomwonyesha mtoto akiwa mtupu.
Seneta wa kihafidhina mwenye ushawishi mkubwa na mshauri wa serikali kwa masuala ya watoto wote wamelielezea tamasha hilo kuwa ni tamsha la ngono ya watoto na wametaka kufungwa kwake.
Mashuhuda wanasema takriban wanaharakati ishirini waliojiita kuwa ni maafsa wa Urusi, walilifunga tamasha hilo mjini Moscow na mmoja kati yao alirembea chupa ya mkojo juu ya baadhi ya picha hizo.
Msimamizi wa tamasha hilo alisema alikuwa analifunga tamasha hilo baada ya kupata vitisho kwa watu wenye nia mbaya.