Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kimbunga kikali kuipiga pwani ya Australia
kimbunga kikali kinatarajiwa kupiga pwani ya Australia ya Queensland muda mfupi pamoja na upepo mkali na mvua kubwa.
Maelfu ya wakazi wameondolewa kutoka miji ya pwani, na kuacha nyumba zao zikijaa maji.
Gavana wa Queensland, Annastacia Palaszczuk, amesema kwa sasa watu wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa na watu hawapaswi kutembea hovyo.
Wafanyakazi elfu mbili wa dharura wanasubiri na kujiandaa kufika katika eneo hilo kutoa msaada kwa kadri itakavyohitajika.
Taarifa za wataalam wa mambo ya hali ya hewa wanasema upepo unatarajiwa kuvuma kwa kilomita 280 kwa saa moja.