Kimbunga kikali kuipiga pwani ya Australia

Mwenendo wa kimbunga hicho katika picha za rada
Maelezo ya picha, Mwenendo wa kimbunga hicho katika picha za rada

kimbunga kikali kinatarajiwa kupiga pwani ya Australia ya Queensland muda mfupi pamoja na upepo mkali na mvua kubwa.

Maelfu ya wakazi wameondolewa kutoka miji ya pwani, na kuacha nyumba zao zikijaa maji.

Gavana wa Queensland, Annastacia Palaszczuk, amesema kwa sasa watu wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa na watu hawapaswi kutembea hovyo.

Tiyari watu wameanza kuondoa bidhaa kwenye maduka yao
Maelezo ya picha, Tiyari watu wameanza kuondoa bidhaa kwenye maduka yao

Wafanyakazi elfu mbili wa dharura wanasubiri na kujiandaa kufika katika eneo hilo kutoa msaada kwa kadri itakavyohitajika.

Taarifa za wataalam wa mambo ya hali ya hewa wanasema upepo unatarajiwa kuvuma kwa kilomita 280 kwa saa moja.