Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uber yatumia ''progamu ya kisiri'' kuhepa wakaguzi
Kampuni ya Magari ya Uber, ya Marekani, imekiri kutumia programu ya kisiri ya kompyuta, kuisaidi kutambua na kuwazuia wakaguzi kupata taarifa,inayotoa ushahidi wowote kwamba inavunja sheria inayoongoza huduma ya usafiri wa texi.
Programu hiyo imeundwa kwa njia ya kipekee, kuwakinga madereva wa kampuni hiyo, dhidi ya watumizi ambao wanaweza kuwawekea mtego kwa lengo la kuwakamata.
Gazeti la The New York Times imefichua kuwa kampuni ya Uber imetumia programu hiyo ya kisiri kuendesha shughuli zake katika miji kama vile Boston na Paris, Hali kadhalika katika mataifa ya Australia, Italia,na China.
Kampuni ya Uber inakabiliwa na tuhuma za ubaguzi kwa misingi ya kijinsia , ushindani mbaya, unaotokana na mtindo wake wa usimamizi na vile vile kuwapunja madereva.