Mshindi wa Oscar kutoka Iran amkosoa Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwelekezi wa filamu raia wa Iran Asghar Farhadi amemkosoa rais wa Marekani Donald Trump na kumtaja kuwa mkosa utu, baada ya filamu yake ya The Salesman, kushinda tuzo la filamu bora ya lugha ya kigeni katika tuzo za Oscar.
Farhai alisusia sherehe lakini aliwakilishwa na watu wawili wenye uraia wa Iran na wenye asili ya Marekani.
"Kuigawanya dunia katika ya Marekani na maadui zetu inaleta hofu," hotuba yake ilisema.

Chanzo cha picha, AFP
Mahakama za Marekani zilizuia marufuku ya kusafiri lakini uongozi wa Trump tena unaandaa amri nyingine kuu.
Marufuku ya awalia iliwazuia kwa muda wahamiaji kutoka nchi saba zenye waislamu wengi duniani.
Mmoja wa wale walioteuliwa kumuakilisha Farhadi ni mhandisi mzaliwa wa Iran ambaye sasa ni mwanasayansi mmarekani wa anga za juu Anousheh Ansari, ambaye alisoma hotuba yake

Chanzo cha picha, Reuters








