Nchi zipi zinaweza kufaidika kwa vita dhidi ya Iran - na zipi zitakazopata hasara kubwa zaidi?

A BBC graphic showing Russian President Vladimir Putin and Chinese President Xi Jinping looking in opposite directions and divided by a photomontage depicting a petrol pump, container ship, warplane, passenger jet, Iranian woman and flag and a plume of black smoke.
    • Author, Marina Daras
    • Nafasi, BBC World Service
    • Author, Stephen Hawkes
    • Nafasi, BBC World Service
  • Muda wa kusoma: Dakika 7

Nchi zipi zinaweza kufaidika kwa vita dhidi ya Iran - na ni zipi zitakazopata hasara kubwa zaidi?

Ni mara chache sana kunakuwa na washindi dhahiri katika vita - na watu wa kawaida mara nyingi hulipa gharama kubwa zaidi. Huku masoko ya kimataifa ya mafuta na misururu ya ugavi ikiwa katika mkanganyiko, baadhi ya nchi duniani kote zinatazamia matokeo mabaya ya kiuchumi - lakini nyingine zinaweza kupata fursa mpya za kimkakati miongoni mwa machafuko hayo.

Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vina madhara makubwa kwa kanda na dunia. Vimesababisha ukosefu wa utulivu katika nchi za Ghuba na kuwalazimu mamia kwa maelfu katika eneo la Mashariki ya Kati kukimbia makazi yao.

Mbali zaidi na eneo la vita, kupanda kwa bei ya mafuta na usumbufu wa usafiri wa baharini katika eneo la Ghuba, hasa ndani na karibu na mlango bahari wa Hormuz, kunaongeza gharama kwa watumiaji na wafanyabiashara.

Lakini ni nchi gani ambazo zinaweza kupata hasara au kunufaika zaidi wakati wa machafuko hayo?

Urusi

Russian President Vladimir Putin, wearing a black suit and red tie, is having a sit down conversation with Iranian Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei, to his right. The Iranian flag can be seen at the back, between the two men.

Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

Maelezo ya picha, Kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei kunaashiria mkwamo mwingine wa kidiplomasia kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Iran ni mshirika mkuu na muhimu wa kijeshi kwa Urusi. Na kuuawa kwa Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei kunaashiria mkwamo mwingine wa kidiplomasia kwa Urusi baada ya kupinduliwa kwa Bashar al-Assad, nchini Syria, na kutekwa kwa Nicolas Maduro na Marekani, nchini Venezuela.

Hata hivyo, mzozo wa Mashariki ya Kati unaweza kuifanya Urusi kunufaika kutokana na vita vinavyoendelea huko Ukraine, kwani vinaelekeza rasilimali za kijeshi za Marekani eneo jingine kando na Urusi.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Kupungua kwa makombora ya Patriot na ndege za kivita za kuzuia makombora kunafaidisha Urusi kwa sababu kunaweka kikomo kile ambacho Ukraine inaweza kupata kutoka kwa washirika wake," Nicole Grajewski, profesa msaidizi katika Kituo cha Mafunzo ya Kisiasa cha Paris kwa Mafunzo ya Kimataifa anaiambia Idhaa ya Kirusi ya BBC.

Kuongezeka kwa mahitaji ya Tehran kwa ndege zisizo na rubani za Shahed za Iran, hata hivyo, hakuna uwezekano mkubwa wa kuathari Urusi nchini Ukraine, wataalam wanasema.

"Urusi ilitegemea Irani kwa ushirikiano wa kiulinzi wakati wa kipindi maalum mwanzoni mwa vita vya Ukraine, wakati Iran ilitoa ndege zisizo na rubani za Shahed, na muhimu zaidi, teknolojia yao ya uzalishaji na leseni za ndege hizi zisizo na rubani, mnamo 2022-2023," Hanna Notte, mkurugenzi wa Eurasia katika Kituo cha Mafunzo ya Kuzuia Kuenea kwa silaha zenye uharibifu mkubwa, huko Marekani, aliiambia BBC News.

"Sasa tuko katika hatua ya vita ambapo Urusi haihitaji Iran kuendelea na vita nchini Ukraine. Urusi inaweza kuzalisha ndege zisizo na rubani za Shahed peke yake."

.

Wakati huo huo, kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz na Iran ambako kumezuia usafirishaji wa mafuta na gesi na kusababisha bei ya mafuta kupanda, inaweza kutoa afueni ya kifedha kwa Urusi, ambayo imekuwa katika hali ngumu kwa sababu ya vita vya Ukraine.

Bajeti ya serikali ya Urusi inategemea nchi hiyo kusafirisha mafuta kwa $59 kwa pipa - lakini sasa, bei ya mafuta ghafi imepanda kwa kiasi kikubwa, hadi karibu $120 kwa pipa kwa wakati mmoja.

Na kutokana na wazalishaji wakuu wa mafuta wa Ghuba kupunguza uzalishaji, Urusi inaweza kuuza nje zaidi kwa masoko muhimu kama vile China na India.

"India hapo awali ilihimizwa kupunguza ununuzi wake wa mafuta nchini Urusi na imefikishwa kiwango cha kama kudharauliwa hivi na Marekani ili kuruhusiwa kununua mafuta ya Urusi tena, angalau kwa mwezi ujao," David Fyfe, mwanauchumi mkuu Argus, kampuni ya kimataifa ya nishati na soko la bidhaa, amesema.

"Na tayari kuna baadhi ya mazungumzo kuhusu kulegeza baadhi ya vikwazo kwa mafuta ya Urusi ili kupunguza baadhi ya matatizo."

China

China bado haijakumbana na athari kubwa kutokana na vita dhidi ya Iran - lakini bado itahisi kusukwasukwa.

Takriban 12% tu ya mafuta yasiyosafishwa yanayoagizwa na China ni ya Iran, kulingana na Kituo cha Sera ya Nishati ya Kimataifa.

Zaidi ya hayo, China imeweka akiba ya mafuta ya kutosha kwa miezi kadhaa na inaweza kwa urahisi kurejea Urusi kwa usaidizi baada ya hapo.

Lakini "sekta ya viwanda inayolenga mauzo ya nje" ya China pia itaathirika, Fyfe anasema.

Takriban asilimia 20 ya pato la taifa la China (GDP) - jumla ya thamani ya bidhaa inazozalisha na huduma inazotoa - mauzo ya nje yamekuwa kichocheo kikuu cha uchumi wake, ambao umedorora kwa sababu ya bei ya majengo na matumizi duni ya ndani.

Usumbufu wa trafiki baharini ndani na karibu na Mlango Bahari wa Hormuz sio tatizo kubwa kwa China - lakini kufika Atlantiki ni muhimu kwa bidhaa za China zinazoelekea Magharibi.

Na kwa upande mwingine wa Rasi ya Arabia, Mlango Bahari wa Bab el-Mandeb, unaounganisha Asia, Ulaya na Afrika, umeshuhudia mashambulizi ya Wahouthi wenye makao yake Yemen, wanamgambo wenye silaha wanaoungwa mkono na Iran.

.

"Kuna uwezekano mkubwa kwamba trafiki ya Bahari ya Shamu itaathiriwa vibaya tena, na meli za mizigo za masafa marefu kutoka Asia zinazotaka kwenda katika bonde la Atlantiki zikielekezwa kusini mwa Afrika na Rasi ya Cape of Good Hope," Fyfe aliambia BBC News.

"Kuna gharama kubwa ya kulipia hilo," Neil Quilliam, mtaalam wa Mashariki ya Kati huko Chatham House, taasisi yenye makao yake mjini London, amesema.

"Inaongeza siku 10 hadi 14 kwa safari. Na kulingana na bidhaa, kwa meli ya wastani, inagharimu takriban $2m za ziada."

Vita dhidi ya Iran huenda vikaipatia China fursa za kidiplomasia, hata hivyo, inapojaribu kujiweka kwa Marekani kama "mpinzani anayeendeleza usawa," Philip Shetler-Jones, kutoka Taasisi ya Huduma za Kifalme ya Uingereza, aliambia BBC News.

Rais wa China Xi Jinping ataendelea kuonyesha sura yake kama kiongozi thabiti na anayetabirika duniani tofauti na Rais wa Marekani Donald Trump.

Na mzozo huo unaweza pia kuwa fursa kwa China "kutafuta vidokezo" juu ya jinsi Trump anaweza kujibu kwa migogoro mingine, ikiwa ni pamoja na Taiwan, kisiwa kinachojitawala ambacho China inadai ni chake.

Uchumi unaoibukia

Kwa kutegemea sana mafuta na gesi ya Mashariki ya Kati, nchi za Kusini Mashariki mwa Asia zinakaribia kuathirika na vita hivyo. Na wengine tayari wamechukua hatua kali za kubana matumizi, wakitumai kupunguza athari za kiuchumi mapema iwezekanavyo.

Nchini Vietnam, bei ya dizeli tayari imepanda kwa 60% tangu kuanza kwa vita - na serikali inaomba kila mtu kufanya kazi nyumbani ikiwa inawezekana.

Nchini Ufilipino, ambayo inaagiza takriban 95% ya mafuta yasiyosafishwa kutoka Mashariki ya Kati, wafanyikazi wa sekta ya umma sasa wanafanya kazi siku nne kwa wiki, isipokuwa wanaofanya kazi katika huduma za dharura.

Masharti kama hayo yameanzishwa nchini Pakistani, isipokuwa kwa wafanyakazi wa benki. Maagizo ya kufanya kazi kutoka nyumbani yametolewa na madarasa ya chuo kikuu kuagizwa kufanyika mtandaoni.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif alisema ni muhimu kuhifadhi na kugawa kwa makini akiba ya mafuta nchini humo.

Nchini Bangladesh, serikali inakabiliana na ununuzi wa bidhaa kunakosababishwa na hofu. Kukiwa na foleni ndefu kwenye vituo vya mafuta, mgao umeanzishwa - lita 10 kwa siku kwa magari na mbili tu kwa pikipiki.

Dozens of motocycle riders queue at a petrol station in Karachi, Pakistan, on the night of 6 March 2026.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vituo vya mafuta vinashuhudia foleni ndefu

Lakini matokeo ya vita yanaweza kuenea zaidi ya uhaba wa mafuta.

Wakulima kote ulimwenguni wanategemea mbolea kuwa na udongo imara na virutubishi vinavyohitajika kukuza chakula na kufanya mazao kustahimili hali ya hewa.

Usumbufu wowote unaweza kusababisha uhaba wa chakula duniani.

Quilliam anaambia BBC News: asilimia "30 ya urea duniani, ambayo hujumuishwa kwenye mbolea, hupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.

Urea hutoka kwa kemikali ya petroli, ambayo hutokana na mchakato wa kufyonza mafuta ghafi. Kwa hivyo ikiwa unaondoa 30% ya urea kwenye soko la kimataifa, hiyo itakuwa na athari ya usalama wa chakula ulimwenguni."

Kufuatia mashambulizi dhidi ya vituo vyake, QatarEnergy, mojawapo ya wauzaji wakubwa wa gesi duniani na mzalishaji wa urea kwa ajili ya mbolea, ilibidi kutangaza hatua ya dharura ambayo inaruhusu makampuni kusimamisha kwa muda uzalishaji na uuzaji wa bidhaa.

"Athari yake inaweza kuonekana katika suala la usalama wa chakula, kwenye mfumuko wa bei ya chakula, miezi sita, tisa baadaye," Quilliam anasema.

"Huenda haijatokea bado - lakini wakati mazao yanatatizika, au wakulima wanapotatizika kupata mbolea yao, matokeo yatashuhudiwa kwa muda mrefu."

Taarifa za ziada za BBC Idhaa ya Kihindi na Elizaveta Fokht, BBC Idha ya Kirusi

Imefasiriwa na Asha Juma