Tetesi za soka Ijumaa: Man City na Barca wafanya mazungumzo juu ya Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City na Barcelona wafanya mazungumzo juu ya mshambuliaji Erling Haaland, kiungo wa kati wa West Ham Mateus Fernandes anafuatliwa na Manchester United, Newcastle wanammezea kiungo wa Monaco Lamine Camara.
Barcelona wamefanya mazungumzo na Manchester City kuhakikisha wanapata fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 25, iwapo atapatikana kwa uhamisho. (Sport - in Spanish)
Hata hivyo, mwakilishi wa Haaland, Rafaela Pimenta, alipuuza uvumi unaomhusisha kiungo huyo na Barcelona kwenye kipindi cha televisheni cha Uhispania. (Times - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Newcastle United na Italia Sandro Tonali, 25, yuko kwenye orodha ya wanaolengwa na Manchester United ya wachezaji kiungo wa kati wanaoweza kufuatiluwa. (Sun)

Chanzo cha picha, West Ham United
Manchester United imekuwa ikimtafuta kiungo wa kati wa West Ham, Mreno Mateus Fernandes, mwenye umri wa miaka 21, ambaye atatafuta uhamisho wa msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo itashushwa daraja. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle imeimarisha juhudi zake za kumsajili kiungo wa Monaco mwenye thamani kubwa kutoka Senegal Lamine Camara, 22, katika miezi ya hivi karibuni. (The I - subscription required)
Meneja wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, huenda akaacha wadhifa wake kama mkuu wa soka wa Red Bull na kurudi kwenye usimamizi kama kocha wa Ujerumani baada ya Kombe la Dunia. (Bild - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Newcastle Kieran Trippier, 35, bado anaweza kupata mkataba mpya huko St James' Park huku Arsenal ikiendelea kumtafuta beki mwenzake wa pembeni Mwingereza Tino Livramento, 23. (Football Insider)
Newcastle wako mbioni kumtafuta mshambuliaji mpya msimu huu wa joto, licha ya kutumia pauni milioni 124 kipindi hicho mwaka jana, huku winga wa Cologne na Ujerumani chini ya umri wa miaka 21, Said El Mala, 19, pia akifuatiliwa na Magpies. (Mail+ - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa kumsajili mshambuliaji mkongwe wa Poland Robert Lewandowski, 37, huku mkataba wake Barcelona ukitarajiwa kuisha msimu huu wa joto. (Tuttosport - in Italian)
Wadadisi wa mambo ya ndani wa Liverpool wamebatilisha uvumi kwamba kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, anaweza kuuzwa Real Madrid baada ya msimu mmoja tu Anfield. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa zamani wa Everton na Burnley, Sean Dyche, anachukuliwa kama mbadala wa Igor Tudor kama kocha wa muda wa Tottenham. (Independent)
Lakini Dyche anaweza kusita kuchukua kazi hiyo na kutaka hakikisho zaidi ya mwisho wa msimu, huku wachezaji wa zamani wa Tottenham Robbie Keane na Ryan Mason wakitarajiwa kuwa na chaguo. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Atletico Madrid wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 26, kwa klabu katika Ligi Kuu ya Uingereza mradi tu watalipa pauni milioni 85, lakini hawatamruhusu kujiunga na Barcelona. (Sport - in Spanish)
Inter Milan wako tayari kuwaacha beki Alessandro Bastoni, 26, na kiungo Nicolo Barella, 29, waondoke msimu huu wa joto iwapo watapata ofa zinazofaa kwa wawili hao wa Italia. (Gazzetta dello Sport - in Italian)















