Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yataka suluhu Israel na Palestina
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema nchi yake inaunga mkono wazo la suluhu ya mataifa mawili katika mgogoro wa Israel na Palestine.
Lakini, Nikki Haley pia amesema utawala wa rais Trump unaangalia uwezekano wa kupatikana kwa suluhu nyengine.
Kwa miaka mingi, Marekani imekuwa ikiunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestine kando na Israel.
Lakini, bwana Trump amesema siku ya Jumatano kwamba hilo hatolisisitizia.
Amesema, mwisho wa siku, ni juu ya pande mbili zinazohasimiana kutatua mgogoro huo.