Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Donald Trump akutana na Benjamin Netanyahu
Rais Trump amemkaribisha waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ikulu ya Marekani, na kusema atafanya kazi kwa bidii kwa kile alichokiita makubaliano ya amani kati ya Israel na Palestine.
Amesema pande zote mbili zitahitajika kuwa na maridhiamo, na kwamba angetaka Israel isitishe kidogo ujenzi wa makazi unaoendelea.
Kwa upande wake, bwana Netanyahu amesema Israel sharti ihakikishe kuwepo kwa usalama katika eneo la linalokaliwa la West Bank.
Amesema hivi sasa kuna fursa kubwa ya kuwepo kwa makubaliano ya amani kwa kushirika wajumbe wengine wa nchi za kiarabu.
Bwana Netanyahu pia amesema anaamini kwamba uongozi wa bwana Trump unatoa fursa ya kihistoria ya kubadilisha kile alichokiita kama kuwepo kwa wimbi la waislamu wenye msimamo mkali.