Moto wa nyika waangamiza mji Chile

Santa Olga

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mjini Santa Olga, nyumba 1,000 zimeteketea kabisa

Mataifa yameanza kutuma wazima moto nchini Chile kusaidia taifa hilo kukabiliana na moto mbaya zaidi katika historia ya taifa hilo.

Urusi imetuma ndege yenye uwezo wa kubeba tani kadha za maji kujaribu kusaidia kuzima moto huo wa nyika.

Moto huo umeenea kwa kasi sana maeneo ya kati ya Chile, ambapo unasaidiwa na upepo mkali, kiwango cha juu cha joto na hali kwamba maeneo hayo yamekabiliwa na kiangazi kwa muda.

Mji Santa Olga, unaopatikana kilomita 240 kusini mwa Santiago umeharibiwa kabisa na moto huo.

Santa Olga, 240

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwiili wa mtu mmoja uliokuwa umeteketea ulipatikana katika mji wa Santa Olga. Watu 6,000 walifanikiwa kutoroka bila majeraha.
San Ramon

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wakazi walitoroka wakiwa na wanyama wao. Hapa, wakazi wanaonekana ndani ya gari, farasi wao akikimbia kuandamana nao nje
Santa Olga, 26 Januari 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watu wengi wameacha bila makao na bila matumaini
Chile. 26 Januari 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Moto huo umeteketeza karibu hektari 238,000 (ekari 588,000) kote nchini Chile. Maafisa wa msitu wanasema moto huo unaendelea kuenea
Llico, 26 Januari 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wazima moto wamekuwa wakiombolewa wenzao watano waliofariki wakikabiliana na moto huo na kuwaokoa wakazi