Atengwa na wazazi kwa kumpenda kijana mweusi

Kijana mweusi Michael Swift na mpenziwe Allie Dowdle
Maelezo ya picha, Kijana mweusi Michael Swift na mpenziwe Allie Dowdle

Mwanafunzi mmoja amechangisha zaidi ya dola 10,000 kupitia mchango wa raia baada ya kudai kwamba mamake na baba walikata uhusiano wake naye kwa kuwa na mpenzi mweusi.

Allie Dowdle anasema wazazi wake walikataa kumpatia fedha kwa sababu hawakupenda uhusiano wake na kijana huyo mweusi.

Allie Dowdle mwenye umri wa miaka 18 anasema wazazi wake walikata uhusiano naye kwa kumpenda kijana mweuzi Michael Swift

Chanzo cha picha, facebook

Maelezo ya picha, Allie Dowdle mwenye umri wa miaka 18 anasema wazazi wake walikata uhusiano naye kwa kumpenda kijana mweuzi Michael Swift

Akiandika katika ukurasa wake wa GoFundMe ,Allie alisema: Nikiwa na umri wa miaka 18 wazazi wangu wamekataa kunifadhili katika maisha yangu ya baadaye ,na kunipokonya raslimali zangu zote.

Babake msichana huyo hatahivyo amekana kwamba sababu ya kukata uhusiano huo ni ile ya ubaguzi wa rangi.

Allie Dowdle anasema kuwa wazazi wake wamemnyima fedha, gari, simu na fedha za kulipia karo kwa kumpenda mpenzi wake Michael swift

Chanzo cha picha, VCSO

Maelezo ya picha, Allie Dowdle anasema kuwa wazazi wake wamemnyima fedha, gari, simu na fedha za kulipia karo kwa kumpenda mpenzi wake Michael swift

Allie anasema kuwa yeye na Michael Swift wamekuwa katika husiano wa kimapenzi kwa takriban mwaka mmoja baada ya kuwaelezea wazazi wake lakini swala hilo likazuka tena baada ya Michael kukutana na wazazi wake msichana huyo.

Anadai kwamba baada ya mkutano huo wazazi wake walimtenga na sasa hawezi kupata fedha alizohifadhiwa ,gari, simu na hawezi kulipia masomo yake.

Kijana mweusi Michael Swift aliyependwa na msichana mweupe Allie Dowdle

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Kijana mweusi Michael Swift aliyependwa na msichana mweupe Allie Dowdle

''Babangu hakunipa sababu nyengine, aliniambia kwamba siruhusiwi kumuona Michael tena'' ,alisema. Kwa nini? kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.

''Sitasahau vile wazazi wangu walivyonikaripia walipoelezea vile walivyokasirishwa nami kwamba ningeweza kutafuta mtu mwengine mzuri zaidi''.

Allie Dowdle anasema kuwa haishi tena na wazazi wake

Chanzo cha picha, facebook

Maelezo ya picha, Allie Dowdle anasema kuwa haishi tena na wazazi wake