Ntaganda adaiwa kuwafunza mashahidi wake

Waendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita wamemshutumu kiongozi wa waasi nchini Congo kwa kuwaingilia mashihidi katika jaribio la kushawishi matokeo ya kesi yake.
Wamesema kuwa uchunguzi uliofanywa katika simu ya Bosco Ntaganda unaonyesha kwamba alikuwa akiwafunza mashahidi wake mbali na kuzuia uchunguzi wa upande wa mashtaka.
Ntaganda aliyepewa jina la utani kama 'The Terminator' amekana mashtaka 18 yanayomkabili ikiwemo mauaji,ubakaji na kuwatumia wanajeshi watoto.

Chanzo cha picha, AP
Kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda ametoa wito wa hatua kali kuchukuliwa ili kulinda uadilifu wa kesi hiyo.








