Uchaguzi Marekani 2016: Ushindi wa Trump kwa ramani

Chanzo cha picha, Reuters
Katika usiku wa uchaguzi wa kuvutia Mgombea wa urais wa Republican, Donald Trump, amepata ushindi baada ya kujizolea kura katika majimbo ambayo awali yalikuwa ni ngome ya Democratic yakiwemo Pennsylvania, Florida, Ohio na Iowa ambayo yalikichagua chama cha Republican.
Huku baadhi ya majimbo yakiwa bado hayajatangaza matokeo, ramani hii chini tinaonyesha ni jinsi gani kura kwa republican zilivyoimarika kote nchini Marekani na hivyo kusukuma uungaji mkono wa Democratic hadi kwenye ngome zake za mwambao wa magharibi na kaskazini magharibi. Kwa ujumla Donald Trump ameshinda kwa 48% ya kura huku Hillary Clinton akipata 47%.
Democratic wamepoteza uungaji mkono eneo la kati la magharibi mwa nchi na maeneo yanayozingira maziwa makuu, pamoja na Kusini mashariki, huku kura za awali zikionyesha wkwamba Bi Clinton alipokea kura kidogo kutoka kwa jamii zisizo za raia kizungu zaidi ya alivyofanya rais Obama katika chaguzi zilizompa ushindi miaka ya 2012 na 2008.
Mgawanyo wa kitaifa wa kura umeshuka kwa karibu pointi tatu ambapo Democratic wamepata 47% ikilinganishwa na 2012, huku mgawo wa Republican wa kura ukiongezeka kwa chini ya pointi moja.









